NAFASI 11 za Kazi Wilaya ya Kondoa July 11-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 11 za Kazi Wilaya ya Kondoa July 11-2024
NAFASI 11 za Kazi Wilaya ya Kondoa July 11-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kupitia kibali cha Ajira chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024, anapenda kuwatangazia wananchi wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuomba nafasi za kazi katika kada zifuatazo:-
NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Jiji la Dodoma July 11-2024
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KONDOA 12-07-2024
✅DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 06)
SIFA ZA KUAJIRIWA.
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (Form Six), Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila
kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA LA II
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi;
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na
- Kufanya usafi wa gari.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 03)
SIFA ZA KUAJIRIWA.
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI).
Awe na Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II
- Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista (incoming correspondence register);
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (outgoing correspondence register);
- Kusambaza majalada kwa Watendaji (action officers);
- Kupokea majalada kwa Watendaji (action officers);
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji;
- Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali
pengine yanapohifadhiwa; na - Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking).
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II (NAFASI 02)
SIFA ZA KUAJIRIWA.
Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika
moja na kupata programu za compyuta za ofisi kama vile:- Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri;
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matuokio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu
wake na ratiba za kazi zingine; - Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wajukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Divisheni/Kitengo/Sehemu
husika; - Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinahusika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wawasilishe maelezo binafsi (Curriculum Vitae) yanayojitosheleza (Detailed
CV) yenye Anuani na Namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
watatu (Referees) wa kuaminika. - Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Sita, Taaluma na cheti cha kuzaliwa. Waombaji watakaowasilisha” Result Slip”,” Statement of Results”,”
Provisional Results” au” Transcripts HAVITAKUBALIKA. - Kwa Waombaji waliosoma nje ya Nchi, Elimu ya Kidato cha Nne au Sita wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
- Kwa waombaji waliosoma Vyuo nje ya Nchi wawasilishe uthibitisho kutoka Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). - Waombaji watakokidhi sifa zinazotakiwa ndio watakaoitwa katika usaili.
- Barua ya maombi iliyosainiwa na Mwombaji inaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili.
- Waombaji wenye mahitaji maalum (special needs/disability) wanatakiwa kuainisha kwenye maombi yao.
- Waombaji watakaowasilisha Taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba. isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 24 Julai, 2024.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti
ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: DEREVA DARAJA II – 6 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa More Details |
2024-07-24 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa More Details |
2024-07-24 Login to Apply |
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa More Details |
2024-07-24 Login to Apply |