NAFASI 12 za Kazi Wilaya ya Mpimbwe July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 12 za Kazi Wilaya ya Mpimbwe July 2024
NAFASI 12 za Kazi Wilaya ya Mpimbwe July 2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.
Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
✅DEREVA II – NAFASI 03
MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA II
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
iv) - Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote,
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
- Kufanya usafi wa Gari,
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – B
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 01
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri,
- Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaeleza wanapoweza
kusaidiwa, - Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari
za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine, - Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu
ya kazi, - Kupokea majalada
na kusambaza kwa maofisa walio katika Divisheni/Kitengo/Sehemu husika, - Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika,
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali,
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katia Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Awe
amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na. Awe amepata mafunzo ya programu za Kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, Power
point, Internet, E-mail na Publisher.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – C
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 02
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye Regista (Incomming Correspondence Register),
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register),
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers),
- Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji
- Kutafuta kumbukumbu/ Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji,
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa,
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe amehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Utunziji wa Kumbukumbu kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa compyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – C
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 3)
KAZI NA MAJUKUMU
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao kuwa mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji
- Kuratibu na kusimamia upangaji na utelekezaji wa Miradi ya Maendeleo
ya Kijiji - Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mkakati wa kuondoa njaa umaskini na kuongeza uzalishaji mali
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Kijiji
- Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko ya migogoro ya Wananchi
- Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
- Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wako
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne au Sita, Astashahada/Cheti NTA/LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Jamii kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mshahara ya Serikali ngazi ya Mshahara itakuwa TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma - Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu
wa kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya
kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
(referees) watatu wa kuaminika; - Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional
Certificate from Respective Boards); - “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato
cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 07 Agost, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe,
S.L.P. 245, MPANDA
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa
‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe More Details |
2024-08-07 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe More Details |
2024-08-07 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe More Details |
2024-08-07 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 6 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe More Details |
2024-08-07 Login to Apply |