RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 14 za Kazi Tarime District Council August 2024

Filed in Ajira by on 29/08/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 14 za Kazi Tarime District Council August 2024

NAFASI 14 za Kazi Tarime District Council August 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa kushirikiana shirika la Amref Health Africa Tanzania kupitia mradi wa “Afya Thabiti” anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.

✅Mtoa Huduma za VVU na UKIMWI Ngazi ya Kituo (Huduma za uchunguzi na upimaji wa VVU – Optimized PITC) Nafasi (4)

MAJUKUMU YA JUMLA:
Kutoa huduma za VVU na UKIMWI ikiwa ni pamoja na ushauri nasaha, uchunguzi wa sifa za upimaji na upimaji wa VVU kwa lengo la kuibua wateja wapya, Kuunganisha wateja wapya kwenye huduma za Kinga, matibabu na matunzo. Ufuatiliaji wa upatikanaji huduma kwa wateja na ushauri nasaha kuhusu ufuasi endelevu wa dawa na vipimo husika hususani upimaji wa kiwango cha VVU kwa wateja wanaotumia ARV.

MAJUKUMU/KAZI MAHUSUSI:

Kutoa elimu kuhusu VVU na UKIMWI, kufanya uchunguzi wa awali kwa lengo la kubaini watu wenye sifa za kupimwa VVU (Screening for eligibility criteria for HTS) kwa wagonjwa wanaohudhuria katika kituo cha matibabu.
Kuandaa mazingira rafiki ya utoaji huduma ya unasihi, uchunguzi wa vigezo vya kupima VVU na upimaji wa VVU kwa wagonjwa wanaofika kituoni kupata huduma Kutoa huduma bora za ushauri nasaha na upimaji wa VVU kwa wateja na wagonjwa wenye sifa wanaohudhuria kituoni na kwenye ngazi ya jamii (Optimized PITC) kwa kuzingatia miongozo husika.

Ufuatiliaji na upimaji wa wateja wa makundi maalum (watoto na vijana wenye umri wa rika barehe) katika vitengo mbalimbali vya huduma katika kituo na kwenye jamii Kutoa huduma ya upimaji kupitia mitandao ya watu wenye maambukizi ya VVU kama vile wenza na washirika wa ngono na wajidunga pamoja na watoto wa kuzaliwa na mama wenye maambukizi ya VVU (Index Testing and Partner Notification Services)

Kutoa huduma za rufaa na uunganishwaji wa wateja kwenye huduma za kinga (Status Neural Approach) na huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye maambukizi ya VVU (Linkage Case Management) Kurekodi na kutoa taarifa ya matokeo ya uchunguzi na upimaji wa VVU kupitia nyenzo husika.

Kuandaa taarifa kwa usahihi na kuziwasilisha kwa wakati kwa msimamizi kulingana na mahitaji.

Kufanya kazi zingine utakazopangiwa na kiongozi/msimamizi wako.

Soma na hii: MAJINA ya Walioitwa kwenye Usaili Mteknolojia Msaidizi Daraja La Ii – Maabara August 2024

SIFA ZA MUOMBAJI

  • Mwombaji awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi
  • Awe na Cheti cha mafunzo ya Utoaji Huduma za Afya ngazi ya Jamii (Certificate of Community Based Health Services), Health Attendant au ngazi nyinginezo zinazohusiana kutoka chuo kinachotambulika kitaifa.
  • Wenye mafunzo ya ziada kuhusiana na unasihi upimaji wa VVU (Certified Non- Lab. Testers) watapewa kipaumbele.
  • Awe na uwezo na uzoefu wa Kutoa ushauri nasaha na kupima VVU, utoaji wa huduma za matibabu ya ARV pamoja ufuatiliaji wa wateja kuhusiana na ufuasi wa dawa na vipimo husika ikiwa ni pamoja na utafutaji wa wateja wanaopotea.
  • Awe na uelewa kuhusu mfumo wa wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na namna unavyofanya kazi, uwezo wa kutumia miongozo na vitendea kazi mbalimbali vinavyotumika katika utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI.
  • Uwezo wa kuongea, kusoma na kuandika Kingereza na Kiswahili kwa ufasaha. Uwezo wa kutunza siri za wateja/wagonjwa na taarifa zote zilizopo katika mifumo ya taarifa za wateja/wagonjwa.
  • Uwezo wa kutoa huduma kwa watu wote bila unyanyapaa au ubaguzi Awe mtu mwenye kukubalika na watu kwenye ngazi ya kituo na jamii

✅Mtoa Huduma za VVU na UKIMWI Ngazi ya Jamii (Huduma Mkoba na upimaji wa VVU kwa Makundi maalum- Community Based HTS providers) Nafasi (2)

MAJUKUMU YA JUMLA:

Kwa kushitikiana na watoa huduma wengine ngazi ya jamii, kutoa huduma za VVU na UKIMWI ikiwa ni pamoja na ushauri nasaha, upimaji wa VVU kwa lengo la kuibua wateja wapya, Kuunganisha wateja wapya kwenye huduma za Kinga, matibabu na matunzo. Utoaji wa dawa kinga na Ufuatiliaji wa upatikanaji huduma kwa wateja na ushauri nasaha kuhusu ufuasi endelevu wa dawa na vipimo husika hususan upimaji wa kiwango cha VVU kwa wateja wanaotumia ARV.

MAJUKUMU/KAZI MAHUSUSI:

  • Kutoa elimu kuhusu VVU na UKIMWI, kufanya uchunguzi wa awali (Screening for eligibility criteria for CBHS) kwa lengo la kubaini watu walio katika hatari ya kupata maambukizi kama vile makundi maalum, wenza na watoto wa WAVIU na wote wenye sifa za kupimwa VVU na kupata huduma mbalimbali za kinga dhidi ya maambukizi ya VVU
  • Kuandaa mazingira rafiki ya utoaji huduma ya unasihi, uchunguzi wa vigezo vya kupima VVU na upimaji wa VVU kwa watu wenye sifa katika jamii husika
  • Kutoa huduma bora za ushauri nasaha, upimaji wa VVU na dawa kinga kwa wateja wenye sifa hususan walio katika makundi maalum Ufuatiliaji na upimaji wa wateja wa makundi maalum (watoto na vijana wenye umri wa rika barehe) katika jamii
  • Kutoa huduma ya upimaji kupitia mitandao ya watu wenye maambukizi ya VVU kama vile wenza na washirika wa ngono, wajidunga pamoja na watoto wa kuzaliwa na mama wenye maambukizi ya VVU (Index Testing and Partner Notification Services)
  • Kutoa huduma za rufaa na uunganishwaji wa wateja kwenye huduma za kinga na huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye maambukizi ya VVU (Linkage Case Management)
  • Kurekodi na kutoa taarifa ya matokeo ya uchunguzi na upimaji wa VVU kupitia nyenzo husika.
  • Kuandaa taarifa kwa usahihi na kuziwasilisha kwa wakati kwa msimamizi kulingana na mahitaji.
  • Kufanya kazi zingine utakazopangiwa na kiongozi/msimamizi wako.

SIFA ZA MUOMBAJI

  • Mwombaji awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi
  • Awe na Cheti cha mafunzo ya Utoaji Huduma za Afya ngazi ya Jamii (Certificate of Community Based Health Services), Health Attendant au ngazi nyinginezo zinazohusiana kutoka chuo kinachotambulika kitaifa.
  • Wenye mafunzo ya ziada kuhusiana na unasihi upimaji wa VVU (Certified Non- Lab. Testers) watapewa kipaumbele.
  • Awe na uwezo na uzoefu wa Kutoa ushauri nasaha na kupima VVU, utoaji wa huduma za matibabu ya ARV pamoja ufuatiliaji wa wateja kuhusiana na ufuasi wa dawa na vipimo husika ikiwa ni pamoja na utafutaji wa wateja wanaopotea.
  • Awe na uelewa kuhusu mfumo wa wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na namna unavyofanya kazi, uwezo wa kutumia miongozo na vitendea kazi mbalimbali vinavyotumika katika utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI.
  • Uwezo wa kuongea, kusoma na kuandika Kingereza na Kiswahili kwa ufasaha.
  • Uwezo wa kutunza siri za wateja/wagonjwa na taarifa zote zilizopo katika mifumo ya taarifa za wateja/ wagonjwa.
  • Uwezo wa kutoa huduma kwa watu wote bila unyanyapaa au ubaguzi Awe mtu mwenye kukubalika na watu kwenye ngazi ya kituo na jamii

✅Mtoa Huduma za VVU na UKIMWI Ngazi ya Kituo/Jamii – ufuatiliaji wa wateja (CHW/MATT TRACKER) Nafasi (8)

MAJUKUMU YA JUMLA:
Kutoa huduma za VVU na UKIMWI ikiwa ni pamoja na ushauri nasaha na upimaji wa VVU kwa lengo la kuibua wateja wapya, Kuunganisha wateja wapya kwenye huduma za Kinga, matibabu na matunzo. Ufuatiliaji wa upatikanaji huduma kwa wateja na ushauri nasaha kuhusu ufuasi endelevu wa dawa na vipimo husika hususan upimaji wa kiwango cha VVU kwa wateja wanaotumia ARV.

MAJUKUMU/KAZI MAHUSUSI:

  • Ujazaji bora wa nyenzo za ufuatiliaji wateja wanaohudhuria klinic (Appointment register) na mfumo wa kielekronic wa utunzaji takwimu (database) ili kubaini wateja wasiohudhuria kliniki kwa wakati (MISAP) au wanaopotea (LTFU)
    Kutumia taarifa za mifumo ya utunzaji wa kumbukumbu za wateja ili kutambua na kuchambua majalada ya wateja waliopotea (MISAP/LTFU)
  • Kufuatilia, kutafuta wateja wanaopotea kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na simu au ufuatiliaji wa wateja nyumbani.
  • Kurekodi na kutoa taarifa ya matokeo ya ufuatiliaji wa wateja Ufuatiliaji wa wateja (watoto na wenye umri barehe) katika vitengo mbalimbali vya huduma na matunzo na kurudisha kwenye huduma wanaopotea.
    Kutoa huduma za rufaa za ndani na nje ya kituo ili kuwezesha upatikanaji wa huduma endelevu
  • Ufuatiliaji na utoaji wa taarifa za vifo vitokanavyo na VVU na UKIMWI Kutoa elimu kuhusu VVU na UKIMWI, kufanya uchunguzi wa awali kwa lengo la kutambua watu wenye sifa za kupimwa VVU (Screening for eligibility criteria for HTS) kwa wagonjwa wanaohudhuria katika kituo cha matibabu.
  • Kutoa huduma bora za ushauri nasaha na upimaji wa VVU kwa wateja na wagonjwa wenye sifa wanaohudhuria kituoni na kwenye ngazi ya jamii (Optimized PITC) kwa kuzingatia miongozo husika.
  • Kutoa huduma ya upimaji kupitia mitandao ya watu wenye maambukizi ya VVU kama vile wenza na washirika wa ngono na wajidunga pamoja na watoto wa kuzaliwa na mama wenye maambukizi ya VVU (Index Testing and Partner Notification Services)
  • Kutoa huduma za rufaa na uunganishwaji wa wateja kwenye huduma za kinga, tiba na matunzo kwa watu wenye maambukizi ya VVU (Linkage Case Management)
  •  Kuandaa taarifa kwa usahihi na kuziwasilisha kwa wakati kwa msimamizi kulingana na mahitaji.
  • Kufanya kazi zingine utakazopangiwa na kiongozi/msimamizi wako.

SIFA ZA MUOMBAJI

  • Mwombaji awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi
  • Awe na Cheti cha mafunzo ya Utoaji Huduma za Afya ngazi ya Jamii (Certificate of Community Based Health Services) au ngazi nyinginezo zinazohusiana kutoka chuo kinachotambulika kitaifa.
  • Wenye mafunzo ya ziada kuhusiana na utoaji wa huduma za afya/VVU na UKIMWI watapewa kipaumbele.
  • Awe na uwezo na uzoefu wa Kutoa ushauri nasaha na kupima VVU, utoaji wa huduma za matibabu ya ARV pamoja ufuatiliaji wa wateja kuhusiana na ufuasi wa dawa na vipimo husika ikiwa ni pamoja na utafutaji wa wateja wanaopotea.
  • Awe na uelewa kuhusu mfumo wa wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na namna unavyofanya kazi, uwezo wa kutumia miongozo na vitendea kazi mbalimbali vinavyotumika katika utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI.
  • Uwezo wa kuongea, kusoma na kuandika Kingereza na Kiswahili kwa ufasaha. Uwezo wa kutunza siri za wateja/wagonjwa na taarifa zote zilizopo katika mifumo ya taarifa za wateja/wagonjwa.
  • Uwezo wa kutoa huduma kwa watu wote bila unyanyapaa au ubaguzi
  • Awe mtu mwenye kukubalika na watu kwenye ngazi ya kituo na jamii

MASHARTI YA JUMLA

  • Kwa nafasi zote zilizoainishwa hapo juu (Optimized PITC, Community Based HTS providers na CHW/MATT – Trackers), watoa huduma hawa watalipwa posho ya kila mwezi ya Tsh 200,000/=
  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Details Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana wakati wote na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na wadhamini (Referees) wasiopungua watatu.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Taaluma mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • (Diploma, Certificates, – Cheti cha Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate)
    “Testimonial”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao viwevimehakikiwa na kuthibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Iwapo waombaji watawasilisha taarifa zisizo sahihi (kughushi) wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 06/09/2024. Saa 9:30 Alasiri.

MUHIMU:-
KumbukakuambatishabaruayakoyamaombiyakaziiliyosainiwapamojanaVyetivya Elimu,
aidhaanuaniyabaruahiyoielekezwekwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
S.L.P. 16, TARIME.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yatumwe Kupitia Posta Kwa Address tajwa, ama kwa mkono Masjara ya wazi ofisi ya Mkurungezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioelekezwa katika tangazo hili
HAYATAPOKELEWA.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.