RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Rombo July 18-2024

Filed in Ajira by on 18/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Rombo July 18-2024

NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Rombo July 18-2024

NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Rombo July 18-2024

NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Rombo July 18-2024,Halmashauri ya Wilaya ya Rombo imepokea kibali cha ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Kupitia kibali hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo anatangaza nafasi na anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa kujaza nafasi zifuatazo :-

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 10

MAJUKUMU YA KAZI

  • Afisa Masuhuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji,
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji,
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji,
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji,
  • Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu,
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na
    kuongeza uzalishaji mali,
  • Mwenyekiti wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji.
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji,
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji,
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi,
  • Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.

✅MTUNZA KUMBUKUMBU MSAIDIZI DARAJA LA II – NAFASI 05

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye Regista (Incoming
    Correspondence Register).
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register)
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers)
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji
  • Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji.
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/ kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.

NGAZI YA MISHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali – TGS C.

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao.
  • Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma.
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
    SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 31 Julai, 2024.

MUHIMU. Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa na ielekezwe kwa anuani ya; –
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Rombo,
S.L.P 52,
ROMBO

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira(Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.