RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Tanganyika July 11-2024

Filed in Ajira by on 11/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Tanganyika July 11-2024

NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Tanganyika July 11-2024

NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Tanganyika July 11-2024

NAFASI 15 za Kazi Wilaya ya Tanganyika July 11-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amepokea Kibali cha Ajra mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 ya tarehe 25.06.2024. Hivyo, anawatangazia wananchi wote wenye sifa kuomba nafasi mbalimbali za kazi. Nafasi husika ni kama zifuatavyo; –

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA 11-07-2024

✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI (3)

MAJUKUMU YA KAZI:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
  • Kufanya matengenezo madogomadogo ya magari;
  • Kujaza na Kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
  • Kufanya usafi wa gari; na
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.

SIFA ZA KUAJIRIWA:
Awe na cheti cha kidato cha nne (Form IV) na Leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe
amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Ufundi stadi (VETA) au NIT au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS B.

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI NNE (4)

MAJUKUMU YA KAZI:

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine;
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
  • Kupokea Majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya Vikao mbalimbali; na
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.

SIFA ZA KUAJIRIWA:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili. Aidha, wawe wamefalu somo la hati mkato ya Kiswahili na Kingereza
maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za Ofisi kama vile; Word, Excel, Power Point, Internet, Email na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS C.

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI TATU (3)

MAJUKUMU YA KAZI:

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye Rejista (incoming correspondence register);
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register);
  • Lusambaza majalada kwa watendaji (action Officers);
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji;
  • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada yanayohitajika kwa watendaji;
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (racks/filling Cabinet) au mahali pengine yanapohifadhiwa; na
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (File Tracking).

SIFA ZA KUAJIRIWA:
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe amehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA
Level 6) katika fani ya Masjala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa compyuta.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS C.

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI TANO (5)

MAJUKUMU YA KAZI:

  • Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa Serikali ya Kijiji;
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa
    utawala bora katika Kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji;
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika
    kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalamu katika Kijiji;
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
  • Kusimmaia utungaji wa sgeria ndogo za Kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

SIFA ZA KUAJIRIWA:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada/Cheti katika fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa
kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS B.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi
    miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha
    kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya
    Ajira Katika Utumishi waUmma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae)
    yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (Email address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi
    yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria /Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia
    kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa
    za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, –
    Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 23 Julai, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,
S.L.P. 1,
MPANDA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya
Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.