RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 16 Za Kazi Wilaya ya Iramba July 2024

Filed in Ajira by on 26/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 16 Za Kazi Wilaya ya Iramba July 2024

NAFASI 16 Za Kazi Wilaya ya Iramba July 2024

NAFASI 16 Za Kazi Wilaya ya Iramba July 2024

NAFASI 16 Za Kazi Wilaya ya Iramba July 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe
25/06/2024 pamoja na Kibali cha Ajira Mbadala chenye Kumb Na.FA.228/613/01/D/022 cha
tarehe 21 Juni,2024 kwa mchanganuo ufuatao: –

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III –NAFASI (5)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Afisa masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali za Kijiji;
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na Mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi
    wa Utawala bora katika Kijiji;
  • Katibu wa Mikutano na kamati za Halmashauri ya Kijiji;
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na taratibu za kanuni za kudumu za Utumishi wa
    Umma;
  • Kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza Mikakati ya kuondoa njaa,
    umasikini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya Kitaalam katika Kijiji;
  • Kusimamia kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
  • Mwenyekiti wa Kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na Migogoro ya Wananchi; na
  • Lusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji; na

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwenye Elimu ya kidato cha nne (IV) au sita (VI); aliyehitimu Mafunzo ya
Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo. Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya jamii na Sanyansi ya Sanaa kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. Astashahada yenye alama ya

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II -– NAFASI 4

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuchapa barua, Taarifa na Nyaraka za kawaida;
  • Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaeleza sehemu wanazoweza kushughulikiwa;
  • Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni na tarehe za vikao;
  • Kusaidia na kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, Nyaraka au kitu chochote
    kinachohitajika katika shughuli za Ofisi;
  • Kusaidia kupokea majalada na kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo;
    na
  • Kutekeleza kazi zozote atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi

SIFA ZA MUOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutokakatia Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100
kwa dakika moja na. Awe amepata mafunzo ya programu za Kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye Register (Incoming correspondence Register);
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing correspondence Register);
  • Kusambaza majalada kwa Watendaji (Action Officers);
  • Kupokea majalada yanayorudi Masjala toka kwa Watendaji;
  • Kutafuta Kumbukumbu/ Nyaraka/Majalada na Watendaji;
  • Kurudisha Majalada kwenye Subaka/Kabati la majalada (Racks/filling Cabinets) au
    mahali pengine yanapohifadhiwa; na
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (File Tracking)

SIFA ZA MUOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu
Stashahada (NTA level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka Vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 3

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kukagua Gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa Gari;
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya Gari;
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari “Log-book”;
  • Kufanya usafi wa gari; na
  • Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na Mwajiri wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwenye Elimu ya kidato cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia Kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali, Awe amehudhururia mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basic Driving course) yanayotolewa na Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au
Chuo kingine linachotambuliwa na Serikali

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na
    usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
    kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
    kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum
    Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
    Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu
    wa kuaminika Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective
    Boards);
  • Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato
    cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
    isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
    Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
    kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 8 Agosti, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Iramba,
S.L.P. 355,
Kiomboi-Iramba.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya
Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.