RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 16 za Kazi Wilaya ya Kyerwa July 16-2024

Filed in Ajira by on 16/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 16 za Kazi Wilaya ya Kyerwa July 16-2024

NAFASI 16 za Kazi Wilaya ya Kyerwa July 16-2024

NAFASI 16 za Kazi Wilaya ya Kyerwa July 16-2024

NAFASI 16 za Kazi Wilaya ya Kyerwa July 16-2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa amepokea kibali cha Ajira chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 na kibali cha ajira Mbadala chenye Kumb. Na. FA.228/613/01/B/012 cha tarehe 22 Aprili, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KYERWA 16-07-2024

Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi ya nafasi mbalimbali kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa:-

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 03

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye regista(Incoming
    correspondence register).
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (Outgoing correspondence register).
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers).
  • Kupokea majalada yanayorudi masijala toka kwa watendaji.
  • Kupokea majalada kwa watendaji (Action Officers).

SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe amehitimu Eimu ya kidato na nne [IV] au kidato cha sita [VI] na awe na Stashahada [NTA level 6] katika fani ya masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali, mwenye ujuzi wa kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGS C1

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI (KATIBU MAHSUSI ) II – NAFASI 02)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
  • Kupokea wageni na kuwasili shida zao na kuwaelekeza sehemu anapoweza kushughulikiwa
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazoitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/ Kitengo /sehemu husika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali, na
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.

SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe amehitimu Kidato cha nne na mwenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza
maneno 100 kwa dakika moja na kupata Program za Kompyuta za ofisi kama vile;Word, Excel, Power Point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara ni TGS C1.

✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 04

KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA LA II

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
  • Kufanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari, na
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu na mwenye cheti cha kidato cha Nne ( Form IV ). Awe na leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGS B1.

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 07

KAZI NA MAJUKUMU

  • Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya kijiji na Kamati zake katika kupanga mipango ya
    maendeleo na utekelezaji wake.
  • Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya kijiji na Kamati zake katika kupanga mipango ya
    maendeleo na utekelezaji wake.
  • Mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala Bora katika kijiji.
  • Kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji
  • Kuratibu Sera na kanuni pamoja na kusimamia utekelezaji wa mipango ya kijiji.
  • Kuratibu na kusimamia matumizi Bora ya nguvu kazi.
  • Kusimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO’S
    zilizopo katika kijiji.
  • Kuratibu vikao vya maendeleo ya kijiji vinavyowahusisha wananchi na wataalamu walio katika kijiji chako.
  • Kusimamia na kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika kijiji chako.
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
  • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji; na
  • Kuwajibika kwa Mtendaji wa Kata

SIFA ZA MWOMBAJI

Awe na Elimu ya kidato cha nne (Form IV) au cha sita (Form VI) aliefuzu mafunzo ya Astashahada (NTA – level 5) katika moja ya fani zifuatazo: – Utawala, Sheria, Maendeleo ya jamii, Sayansi ya Jamii, Usimamizi wa Fedha na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGS B1

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa aajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti ya kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Testmonials” “Provisional Results”. Statement of Results”, hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.CCA.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Julai, 2024 saa 9.30 Alasiri.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KYERWA,
S.L.P 72,
KYERWA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

DONWLOAD PDF DOCUMENT

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.