RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 16 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukombe July 05-2024

Filed in Ajira by on 05/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 16 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukombe July 05-2024

NAFASI 16 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukombe July 05-2024, Ajira 16 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Bukombe July 05-2024, Nafasi za Kazi za za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Bukombe July 07-2024.

NAFASI 16 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukombe July 05-2024

NAFASI 16 za Watendaji wa Vijiji Wilaya ya Bukombe July 05-2024, Ajira 16 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Bukombe July 05-2024, Nafasi za Kazi za za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri Wilaya ya Bukombe July 07-2024.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024.

Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma
maombi kwa kada Nafasi 16 za Mtendaji Wa Kijiji Daraja la III kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (“Village Executive” NAFASI 16)

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti au NTA level 5 katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala,
Sheria, Elimu ya Jamii, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III.

  • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
  • Kusimamia Ulinzi na Utawala Bora kwa Raia na mali zao.
  • Kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa Utawala bora katika Kijiji.
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika Kijiji
  • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na
    kuongeza uzalishaji mali.
  • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
  • Kuwa mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Kijij
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi
  • Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji na;
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 nausiozidi miaka 45 isipo kuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavuwalionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Adress) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
    kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
    kuzingatia sifa za kazi husika
    Postgraduate/Degree/Advanced
    Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na
    cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional
    Certificate from Respective Boards).
  • Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
    katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18 Julai, 2024.

MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 02,
BUKOMBE.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa
ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani
hii pia inapaikana kwenye Tovuti ya Sekretariet ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , ,

Comments are closed.