NAFASI 18 za Kazi Kusulu Town Council August 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 18 za Kazi Kusulu Town Council August 2024
NAFASI 18 za Kazi Kusulu Town Council August 2024,Mkurugenzi wa Mji Kasulu amepokea kibali cha ajira mpya kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumbu Na. FA.228/613/01/C/021 cha tarehe 25 Juni, 2024.
Hivyo watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo;
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (NAFASI 2)
MAJUKUMU YA KAZI.
- Kuchapa barua, taarifa au nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa .
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miradi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika Utekelezaji wa majukumu ya kazi
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Vitengo/Sehemu husika.
- Kukusanya, Kutunza na Kuyarejesha Majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word,Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali ni, TGS C.
✅MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III (NAFASI 15).
MAJUKUMU YA KAZI.
- Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa Serikali ya Mtaa;
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Mtaa;Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya Mtaa;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Mtaa;
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na
Kuongeza uzalishaji mali; - Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalamu katika Mtaa;
viii.Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Mtaa; - Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika Mtaa;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Mtaa; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
SIFA ZA MWOMBAJI.
Mwombaji awe na Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV), au Kidato cha Sita (Form VI), aliyehitimu mafunzo katika ngazi ya cheti (NTA LEVEL 5), katika moja ya fani zifuatazo;- Utawala, Sheria, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) au chuo kingine chochote kinachotambulika na
Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali ni, TGS B.
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 1)
MAJUKUMU YA KAZI.
- Kuorodhesha kwenye rejesta barua zote zinazoingia Masjala (Incoming
Correspondence Register) - Kuorodhesha kwenye rejesta barua zinazotoka nje ya Halmashauri (Outgoing Correspondence Register).
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji (Action Officers)
- Kutafuta kumbukumbu au nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji.
- Kurudisha majalada kwenye Shubaka Kabati la Majalada (Racks/Filling Cabinets) au mahala pengine yanapohifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)
NAFASI 18 za Kazi Kusulu Town Council August 2024
SIFA ZA MWOMBAJI.
Mwombaji awe na Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI) aliyehitimu na kupata cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI) na kuhitimu mafunzo ya Stashahada (Diploma) (NTA LEVEL 6) katika Fani ya Utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA.: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali ni, TGS C.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa Kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwaajili
ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma - Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wa
kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao.
- Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Diploma/Certificate, Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma. - Testimonials, “Provision Results”, “Statements of Results”, hati ya matokeo ya kidato cha Nne na Sita HAVITAKUBALIWA
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22/08/2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Mji Kasulu
S.L.P 475
KASULU.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anwani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA