NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Missenyi July 12-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Missenyi July 12-2024
NAFASI 18 za Kazi Wilaya ya Missenyi July 12-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu – ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia baru ayenye Kumb. Na. FA.97/228/01/09 ya tarehe 25.06.2024. Hivyo anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo:-
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MISENYI 12-07-2024
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI (09)
MAJUKUMU YA KAZI
- Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa rai ana mali zao, kuwa mlinzi wa
amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji. - Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya
maendeleo ya Kijiji. - Kuwa katibu wa mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na
kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya
kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali - Kuwa kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
- Kuwa Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika Kijiji
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya kidato cha IV, au VI aliyehitimu mafunzo ya Astashahada / cheti NTA LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo: – Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa katika Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara wa TGS B
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (NAFASI 02)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida;
- Kusaidia kupokea wageni na kuwasili shida zao, na kuwaelekeza
sehemu wanapoweza kushughulikiwa; - Kusaidia kutunza taarifa / kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba ya kazi zingin
zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi; - Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au
kituchochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini; - Kusaidia kupokea majalada kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo na kuyasanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu
zinazohusika; - Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa ampangiwa na msimamizi wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne na mwenye stashahada (Diploma) ya uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno
100 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile;Word, Excel, Power Point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Mshahara utalipwa kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS C.
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 03)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye regista(Incoming correspondence register).
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (Outgoing correspondence register).
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masijala toka kwa watendaji.
- Kupokea majalada kwa watendaji (Action Officers).
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Eimu ya kidato na nne [IV] au kidato cha sita [VI] na awe na Stashahada [NTA level 6] katika fani ya masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali, mwenye ujuzi wa
kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Mshahara utalipwa kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS C.
✅DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 4)
KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA LA II
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama
wa gari. - Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
- Kufanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kufanya usafi wa gari, na
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu na mwenye cheti cha kidato cha Nne ( Form IV ). Awe na leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka bila kusababisha ajali.Na awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic
Driving Course) yanayotolewa na chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya Mshahara wa TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Mwombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na
usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini. - Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa aajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji aambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anawani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti ya kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Testmonials” “Provisional Results”. Statement of Results”, hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.CCA.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 23, Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI,
S.L.P 38,
KYAKA – MISSENYI
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment
Portal’)
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: DEREVA DARAJA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi More Details |
2024-07-26 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi More Details |
2024-07-26 Login to Apply |
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi More Details |
2024-07-26 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 9 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi More Details |
2024-07-26 Login to Apply |