NAFASI 2 Za Mtendaji wa Kijiji Halmashauri ya Mji Nanyamba May 22-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 2 Za Mtendaji wa Kijiji Halmashauri ya Mji Nanyamba May 22-2024
NAFASI 2 Za Mtendaji wa Kijiji Halmashauri ya Mji Nanyamba May 22-2024, Nafasi za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Mji Nanyamba Leo May 22-2024, Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji May 2024, Nafasi za Kazi Kutoka Halmashauri ya Mji Nanyamba May 2024.
Halmashauri ya Mji Nanyamba imepata idhini ya utekelezaji wa Kibali cha Ajira Mbadala chenye Kumb. Na.FA.228/613/01/B/084 cha Tarehe 22/April/2024 kwaaajili ya kuajiri
watendaji wa Vijiji wawili (2).kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Hivyo, Mkurugenzi wa Mji Nanyamba anawatangazia watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Mji Nanyamba, kuomba nafasi za kazi zifuatazo kuanzia leo tarehe 22/05/2024:
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – TGS B (Nafasi 2)
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa awe na elimu ya Kidato cha Nne (IV) au sita (VI)
aliyehitimu mafunzo ya cheti (Astashahada) katika moja ya Fani zifuatazo:
Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI/ MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI
- Afisa masuuli na Mtendaji wa Serikali za kijiji.
- Kusimamia ulinzi wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na usimamizi wa utawala bora katika Kijiji.
- Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji.
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
- Kutafsiri na kusimamia sera na taratibu
- Kuandaa taarifa za utekelezaji na kazi katika eneo lake na kuhamasisha uchumi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa umaskini na kuongeza
uzalishaji mali. - Kiongozi mkuu wa Idara na Vitengo vya kitaaluma katika Kijiji.
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za Kijiji.
- Kupokea, kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi
- Kusimamia ukusanyaji wa mapato katika Kijiji.
- Kuandaa na kutunza Rejesta ya wakazi wote wa Kijiji.
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji na Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
- Pamoja na kazi zingine utakazopangiwa na Mwajiri wako.
MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara ni TGS B1.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na siobpungufu ya Miaka 18.
- Waombaji wenye ulemavu wnahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili
ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. - Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe (Email address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Matokeo ya muda (Provisional/Testimonials/Statement of results) havitakubaliwa.
- Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Wombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya
nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia waliokobkatika Utumishi wa Umma wasiombe na Wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mafunzo mbali
mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (NACTE na NACTE)
- Wasilishaji wa Taarifa na Sifa za
kughushi, wahausika watachukuliwa hatua za kisheria
Barua ya maombi itatakiwa iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Jumanne, tarehe 04 Juni, 2024.
MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe
kwa;
Maombi yote yatumwe kwenye anuani ifuatayo;
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Nanyamba,
S.L.P 1490,
NANYAMBA-MTWARA.
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 2 POST Employer: Halmashauri ya Mji Nanyamba More Details |
2024-06-04 Login to Apply |
Halmashauri ya Mji Nanyamba ilianzishwa rasmi mwezi Julai, 2015 kwa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) namba 8 ya mwaka 1982 kwa Tangazo la Serikali Namba 220 la tarehe 05/06/2015. Madhumuni halisi ya kuanzishwa Kwa Halmashauri ya Mji Nanyamba ni kusogeza karibu na wananchi huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii zikiwemo sekta za Maji, kilimo, Elimu, Barabara, Afya pamoja na kuboresha miundombinu iliyopo kwa manufaa ya wananchi wa Nanyamba.
MIPAKA
Halmashauri ya Mji Nanyamba ni miongoni mwa Halmashauri tatu zilizo katika Wilaya ya Mtwara. Kwa upande wa Kaskazini Mashariki inapakana na Halmashauri ya Wilaya Mtwara. Magharibi inapakana na Wilaya ya Tandahimba na Mkoa wa Lindi. Kusini Nchi ya Msumbiji. Makao Makuu ya Halmashauri yapo katika kata ya Nanyamba, Jimbo la uchaguzi lipo moja la Nanyamba ,Tarafa 3 kata 17 vijiji 87 mitaa 9 na vitongoji 323.
ULINZI NA USALAMA
MAHAKAMA
Halmashauri ya Mji Nanyamba inatumia Mahakama ya Wilaya ya Mtwara pamoja na Mahakama za Mwanzo mbili ambazo ni Nanyamba na Kitaya
HALI YA UPATIKANAJI WA CHAKULA.
Kwa kipindi hiki Wananchi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba wanaendelea na shughuli ya kilimo cha mazao ya muda mfupi kama njugu mawe, karanga, mpunga, mbaazi, mahindi, mtama, kunde, ufuta pamoja na maandalizi ya mashamba ya mikorosho hasa kwa kazi za upuluziaji wa dawa za magugu.
Aidha vyakula vya aina mbalimbali vinapatikana majumbani, kweye masoko na magengeni. Vyakula vya aina ya wanga vinavyopatikana ni pamoja na Mchele, Makopa (mihogo), Mahindi (sembe) na Mtama. Pia mboga za majani za aina mbalimbali zinapatikana zikiwemo bilinganya, bamia, matembele, mchicha, kisamvu (majani ya muhogo), chainizi na nyanya maji. Baadhi ya Matunda kama nanasi na mastafeli yanapatikana.
HALI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ina barabara zenye urefu wa km 498.85 kuna barabara za Mkoa zenye urefu wa Km. 82.8 na Barabara za Halmashauri ya Mji Nanyamba zenye urefu wa Km 416.05 hivyo kufanya Halmashauri ya Mji wa Nanyamba kuwa na barabara zenye urefu wa km 498.85 Mtandao Huu wa barabara ambao hupitika kipindi chote cha Mwaka. Mtandao huu wa barabara huwasaidia wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa vyombo vya usafiri wa magari ya mizigo, mabasi, baiskeli na Pikipiki.
HALI YA MASOKO NA HADHI ZAKE.
Shughuli za biashara (masoko) zinazopatikana au zinazoendelea ni pamoja na biashara za mazao mchanganyiko, Maduka rejereja, hivyo uwepo wa shughuli hizo umesababisha Halmashauri kupata mapato kupitia tozo mbalimbali kama kodi ya ushuru wa bidhaa, ushuru wa masoko na leseni za biashara.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NAFASI 2 Za Mtendaji wa Kijiji Halmashauri ya Mji Nanyamba May 22-2024, Nafasi za Kazi Kutoka Halmashauri ya Mji Nanyamba May 2024., Nafasi za Kazi za Watendaji wa Vijiji May 2024, Nafasi za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Mji Nanyamba Leo May 22-2024