NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Arusha July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Arusha July 2024
NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Arusha July 2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Arusha 19-07-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha amepokea kibali cha kutekeleza Ikama na Bajeti kwa Ajira Mpya kwa mwaka wa
fedha 2023/2024 chenye Kumb. Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha anawatangazia wananchi wote ambao ni Raia wa Tanzania wenye sifa kuomba nafasi zilizoorodheshwa hapa chini:-
✅DEREVA DARAJA LA II – (NAFASI 7) –
MAJUKUMU YA DEREVA
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safarizote katika daftari la safari na
- Kufanya usafi wa gari
SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI), Awe na Leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B 1.
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II (NAFASI 3)-
MAJUKUMU
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri
- Kupokea Wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa za kumbukumbuka za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa
majukumu ya kazi - Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/ Kitengo/ sehemu husika
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa awe na Elimu ya kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe wamefaulu somo la Hitimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata progamu za kompyuta za Ofisi kama vile; Word Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C 1.
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – (NAFASI 7) –
MAJUKUMU
- Afisa Masuuli na Mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
- Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
- Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalama katika kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.
- Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wake.
SIFA ZA KUAJIRIWA
Waombaji wanatakiwa wawe wenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form Six) aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.
✅DEREVA MITAMBO (PLANT OPERATOR) – (NAFASI 1)-
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuendesha mitambo chini ya usimamizi wa Dereva mitambo mwenye uzoefu.
SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha nne ambao wana leseni Daraja la “G” ya
kuendesha Mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo hiyo, wenye uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda saa (300) au miezi mitatu (3)
bila kusababisha ajali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani – TGOS A
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMU DARAJA II (NAFASI 2) –
MAJUKUMU
- Kutafuta kumbukumbu /nyaraka /majalada yanayohitajika na Watendaji /Action Officers
- Kudhibiti upokeaji na uandikishaji wa kumbukumbu / nyaraka
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming
corresponding registers) - Kuchambua, kuorodhesha na kupanga nyaraka mbalimbali katika masjala kulingana na somo husika (clarification and indexing)
- Korodhesaha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing
corresponding register) - Kusambaza majalada kwa Watendaji/ Action Officers
- Kufuatiliaji mzunguko wa majalada ndani ya taasisi
- Kurudisha majalada kwenye kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa
- Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa Watendaji/ Action Officers
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha sita (Form VI) aliehitimu
mafunzo ya Stashahada /Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kompyuta.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C 1.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu
walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma - Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza
(DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe
ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za
kazi husika. - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
- “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 30 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Arusha,
S.L.P. 2330,
ARUSHA
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika
tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: DEREVA DARAJA II – 7 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Arusha More Details |
2024-07-30 Login to Apply |
POST: DEREVA WA MITAMBO II -ARUSHA DC – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Arusha More Details |
2024-07-30 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Arusha More Details |
2024-07-30 Login to Apply |
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Arusha More Details |
2024-07-30 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 7 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Arusha More Details |
2024-07-30 Login to Apply |