NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Chato July 20-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Chato July 20-2024
NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Chato July 20-2024,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawla Bora chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024. Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada nne (04) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –
✅MSAIDIZI WA MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II NAFASI KUMI (10)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kusaidia kubuni na kupanga mipango na miradi katika eneo lake
- Kusaidia uwezeshaji na uppatikanaji wa mafunzo kuhusu masuala ya maendeleo
katika eneo lake - Kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo
- Kusaidia kutoa elimu kuhusu kazi za kujitegemea katika eneo lake
- Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya jamii kila mwezi kwa uongozi wa Kijiji na kwa msimamizi wake wa kazi.
- Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na kimaendeleo
Kutambua na kuwezesha kaya masikini kuinua Uchumi wao kupitia fursa na rasilimali zinazowazunguka - Kufanya kazi zingine atakazo pangiwa na mkuu wake wa kazi
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha nne/sita aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) ya maendeleo ya jamii kutoka vyuo vya
maendeleo ya jamii au vyuo vingine vinavyotambulika na serikali katika mojawapo ya fani zifuatazo; Maendeleo ya Jamii, Sayansi ya jamii,Masomo ya Maendeleo, Mipango na Usimamizi wa Miradi, Jinsia na Maendeleo, na Maendeleo vijijini.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (“Records Management Assistant II”)
NAFASI 02
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming
correspondence register) - Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista
(outgoing correspondence register) - Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers)
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji
- Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/mafaili yanayohitajika na watendaji.
- Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa Kumbukumbu/nyaraka.
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification and Boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
- Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (File Racks/Cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
- Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
- Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
- Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
SIFAZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliehitimu
mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa
Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA; Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS C
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (“Village Executive”) NAFASI – 4
KAZI NA MAJUKUMU
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji,
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo katika Kijiji
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini
na kuongeza uzalishaji mali. - Mwenyekiti wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
- Kuwa Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Kijiji
- Kupokea, kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji na;
- Kuwajibika kwa Mtendaji wa Kata.
SIFAZA MWOMBAJI
Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti au NTA level 5 katika mojawapo ya fani zifuatazo:
Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS B
✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 04
KAZI NA MAJUKUMU
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kufanya kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari na
- Kufanya Usafi wa Gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atavyoelekezwa na msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) na kupata cheti cha mtihani wa kidato
cha Nne (IV) Awe na leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari
ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (01) bila
kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji
Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS B
MASHARTI YAJUMLA KWAWAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma. - Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Carriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. - Provisional“/ Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
- yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards). - Waombaji walisoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa nabMamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 28 Julai, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe
kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YAWILAYA YA CHATO,
S.L.P 116,
CHATO.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani
hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa “Recruitment Portal
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika
tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.