RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Manyoni July 2024

Filed in Ajira by on 19/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Manyoni July 2024

NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Manyoni July 2024

NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Manyoni July 2024

NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Manyoni July 2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni amepokea kibali cha Ajira mpya
kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.

Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 16

MAJUKUMU YA KAZI

  • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kijiji;
  • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa amani na Msimamizi wa Utawala bora katika kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia Upangaji wa Mipango ya Maendeleo ya kijiji;
  • Katibu wa Mikutano ya Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria, na Taratibu;
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika
    kuandaa na kutekeleza Mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa Wakuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji;
  • Mwenyekiti wa Kikao cha wataalamu waliopo katika kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na Migogoro ya Wananchi;
  • Kusimamia Utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji;
  • Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata; na
  • Pamoja na kazi nyingine atakazopangiwa na mwajiri wake.

SIFA ZA KUAJIRIWA
Mwombaji anatakiwa awe mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Astashahada (Certificate NTA level 5) Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya
Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS B

✅DEREVA DARAJA LA II NAFASI MOJA 1

SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI), Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria Mafunzo ya Msingi ya uendeshaji Magari (Basic Driving
Course) yanayotolewa na vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi;
  • Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na
  • Kufanya usafi wa gari.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi ya Mishahara ya Serikali TGS B

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II (NAFASI 03)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuchapa barua, taarifa, nyaraka za kawaida na za siri;
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa;
  • Kutunza taarifa za Kumbukumbu ya Matukio, Miadi, Tarehe za Vikao, Safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Divisheni/Kitengo/Sehemuhusika;
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga Dondoo na kufanya Maandalizi ya vikao mbalimbali; na
  • Kuandaa Orodha ya Mahitaji ya vifaa vya Ofisi.

SIFA ZA MWAJIRI
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) mwenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata Programu za Kompyuta za Ofisi kama Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-Mail, na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS C

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
    kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
    Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia
    kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
    husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective
    Boards);
  • Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
    HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 01 Agosti, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya wilaya,
S.L.P 60
MANYONI.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.