NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Ruangwa July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Ruangwa July 2024
NAFASI 20 za Kazi Wilaya ya Ruangwa July 2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa amepokea kibali cha Ajira
mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.
Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
✅DEREVA DARAJA II – NAFASI 6
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kufanya na kusambaza nyaraka mbalimbali pale inapohitajika
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
- Kufanya usafi wa gari na
- Kazi nyingine atazopangiwa na Mwajiri.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI) mwenye Leseni ya
udereva daraja “E au C ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Aweamehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Mshahara utalipwa kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali, TGS B.
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
- Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao, na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kusaidiwa; - Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za
vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine; - Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/ Sehemu husika;
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) na kupata cheti cha
Mtihani wa Kidato cha nne (IV) au Kidato cha sita (VI). Awe na Stashahada
(Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na Awe amepata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Power – Point, Internet, Email na Publisher.
NGAZI YA MSHAHARA: Mshahara utalipwa kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali, TGS C
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence register);
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista (outgoing correspondence register);
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers);
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji (Action Officers);
- Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji (Action Officers);
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (ranks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa;
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi (File tracking);
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (IV) na kupata cheti cha
mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe amehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu (Records Management) kutoka vyuo vinavotambuliwa na serikali, pia awe na ujuzi wa kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Mshahara utalipwa kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali, TGS C
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 4.
MAJUKUMU YA KAZI
- Afisa masuuli na Mtendaji mkuu wa Serikali ya kijiji;
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa Amani na usimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya maendeleo ya Kijiji;
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali; - Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu katika Kijiji;
- Kusimamia, Kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
- Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wako.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada (Cheti) NTA Level 5 katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria,
Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya jamii na Sayansi ya Jamii
kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Mshahara utalipwa kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali, TGS B
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail
Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika; - Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za
kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya
nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo; - Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma Pamoja na cheti cha
kuzaliwa vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - “Testimonial”, “Provisioinal Result”,”Statement of result”, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Wapombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA NA NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Waombaji watakao wasilisha taarifa za kughusi, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08 Agosti, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA,
15 BARABARA YA BOMA,
S. L. P 51,
RUANGWA, LINDI.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anauani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ . Anuani hii
inapatikana pia kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa More Details |
2024-08-10 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa More Details |
2024-08-10 Login to Apply |
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa More Details |
2024-08-10 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 6 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa More Details |
2024-08-10 Login to Apply |