NAFASI 21 za Kazi Manispaa Kigoma/Ujiji August 06-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 21 za Kazi Manispaa Kigoma/Ujiji August 06-2024
NAFASI 21 za Kazi Manispaa Kigoma/Ujiji August 06-2024, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, amepata kibali cha Ajira Mpya kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.
Hivyo basi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa watanzania wote wenye sifa, kutuma maombi yao ya kazi kwa nafasi zilizoainishwa hapa chini kama ifuatavyo;-
✅MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA Ill (NAFASI 12).
MAJUKUMU VA KAZI.
- Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa Serikali ya Kijiji;
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na Kuongeza uzalishaji mali;
- Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalamu katika Kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
SIFA ZA MWOMBAJI.
Mwombaji awe na Elimu ya Kidato ella Nne (Form IV), au Kidato cha Sita (Form VI), aliyehitimu mafunzo katika ngazi ya cheti (NTA LEVEL 5), katika moja ya fani zifuatazo;- Utawala, Sheria, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) au chuo kingine chochote kinachotambulika na
Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali ni, TGS B.
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 3)
MAJUKUMU YA KAZI.
- Kuorodhesha kwenye rejesta barua zote zinazoingia Masjala (Incoming
Correspondence Register) - Kuorodhesha kwenye rejesta barua zinazotoka nje ya Halmashauri (Outgoing Correspondence Register).
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji (Action Officers)
- Kutafuta kumbukumbu au nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji .
- Kurudisha majalada kwenye Shubaka Kabati Ia Majalada (Racks/Filling Cabinets) au mahala pengine yanapohifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)
SIFA ZA MWOMBAJI.
Mwombaji awe na Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI) aliyehitimu na kupata cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI) na kuhitimu mafunzo ya Stashahada (Diploma)
(NTA LEVEL 6) katika Fani ya Utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
NGAZI Y A MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali ni, TGS C.
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (NAFASI 1)
MAJUKUMU YA KAZI.
- Kuchapa barua, taarifa au nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa.
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miradl, tarene za VIKao, saran za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika Utekelezaji wa majukumu ya kazi
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika ldaraNitengo/Sehemu husika.
- Kukusanya, Kutunza na Kuyarejesha Majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Awe amefaulu somo Ia Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa
dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI Y A MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali ni, TGS C.
✅DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 5)
MAJUKUMU YA KAZI.
- Kukagua gari kabla na baada ya safari iii kubaini hali ya usalama wa gari,
- Kuwapeleka watumishi sehemu mbalimbali kwenye safari za kikazi,
- Kufanya matengezo madogo madogo ya gari,
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari Ia safari,
- Kufanya usafi wa gari, na
- Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa mud a usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali
NGAZI Y A MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali ni, TGS B.
MASHARTI Y A JUMLA
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa Kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wa
kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya
nafasi ya kazi kwa waajiri wao. - Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Diploma/Certificate, Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer
Certificate, Vyeti vya Kitaaluma. - Testimonials, “Provision Results”, “Statements of Results”, hati ya matokeo ya kidato
cha Nne na Sita HAVITAKUBALIWA - Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19/08/2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi wa Manispaa,
Manispaa ya Kigoma Ujiji,
S.L.P 44,
KIGOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anwani ifuatayo; https://portal.ajira.qo.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’) .
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 3 POST Employer: Halmashauri ya Manispaa Kigoma/Ujiji More Details |
2024-08-19 Login to Apply |
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Manispaa Kigoma/Ujiji More Details |
2024-08-19 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Manispaa Kigoma/Ujiji More Details |
2024-08-19 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA MTAA III – 12 POST Employer: Halmashauri ya Manispaa Kigoma/Ujiji More Details |
2024-08-19 Login to Apply |
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NAFASI 21 za Kazi Manispaa Kigoma/Ujiji August 06-2024