NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Jiji la Dodoma July 11-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Jiji la Dodoma July 11-2024
NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Jiji la Dodoma July 11-2024, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia kibali cha Ajira chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024, anapenda kuwatangazia wananchi wote wenye sifa kujaza nafasi za kazi katika kada zifuatazo:
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA 12-07-2024
✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI (04)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Cheti cha Kidato cha nne (Form IV), Leseni ya udereva Daraja E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe
amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji
wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.
MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA II
- Kukagua magari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama
wa gari - Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (Log
Book) - Kufanya usafi wa gari, na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake
MSHAHARA: Cheo hiki kina ngazi ya Mshahara wa TGS B
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI (04)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe mhitimu wa kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za Kompyuta za Ofisi kama
vile; Word, Excel, Powerpoint, Internet, E – mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa - Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe
za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine. - Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa
majukumu ya kazi - Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika
Idara/Kitengo/Sehemu husika - Kukusanya, kutunza na kuyarjesha majalada na nyaraka sehemu
zinazohusika - Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
MSHAHARA: Cheo hiki kina ngazi ya Mshahara wa TGS C
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI (04)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe mhitimu wa Kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada au NTA Level 6 katika mojawapo ya fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu, Urasimu Ramani (Cartography) au (Geoinformatics), Sheria, au Afya kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming
correspondence register) - Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing
correspondence register) - Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers)
- Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji
- Kutafuta kumbukumbu /nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (racks/filing cabinets) au mahala pengine yanapohifadhiwa
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/ nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and indexing) kwaajili ya matumizi ya ofisi
- Kupanga na kudhibiti nyaraka katika vyumba vya kuhifadhia
kumbukumbu (respositories) - Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka, nk) katika majalada
MSHAHARA: Cheo hiki kina ngazi ya Mshahara wa TGS C
✅MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III – NAFASI 10
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani
zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo – Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III:
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mtaa
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi
wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Mtaa - Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya
maendeleo ya Mtaa - Katibu wa Mikutano katika ngazi ya Mtaa
- Kutasfiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu katika ngazi ya
Mtaa - Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati
ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali - Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na
Nyaraka katika ngazi ya Mtaa - Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya
Wananchi katika ngazi ya Mtaa - Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Mtaa
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
MSHAHARA: Cheo hiki kina ngazi ya mshahara wa – TGS B.
MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na wasiozidi umri wa miaka 45.
- Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi sehemu yoyote katika
Halmashauri ya Jiji la Dodoma - Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma, Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na vyeti vya mafunzo
mbalimbali vinavyohusika. - Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika, pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- “Testimonials”, “Provisional results”, “Statement of results”, Hati ya Matokeo ya Kidato cha nne “result slip” havitakubaliwa.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa tu kama wana Kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji wenye vyeti vya Kidato cha Nne na Cheti cha Taaluma ambao vimepatikana Nje ya Nchi wahakikishe vimehakikiwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE).
- Watakaochaguliwa kufanya usaili watajulishwa tarehe ya usaili kupitia tovuti ya Jiji na mbao za matangazo.
Maombi yote yatumwe kwenye Mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatavyo: –
https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya
Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyandikwa ‘Recruitment Portal’)
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa na ielekezwe kwa anuani ifuatayo: –
Mkurugenzi wa Jiji,
Halmashauri ya Jiji la Dodoma,
1 Mtaa wa CDA,
S.L.P. 1249,
DODOMA.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25 Julai, 2024
DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Jiji la Dodoma More Details |
2024-07-25 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA MTAA III – 10 POST Employer: Halmashauri ya Jiji la Dodoma More Details |
2024-07-25 Login to Apply |
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Jiji la Dodoma More Details |
2024-07-25 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Jiji la Dodoma More Details |
2024-07-25 Login to Apply |
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Jiji la Dodoma July 11-2024