RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Mji Korogwe July 06-2024

Filed in Ajira by on 06/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Mji Korogwe July 06-2024

NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Mji Korogwe July 06-2024

NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Mji Korogwe July 06-2024

NAFASI 22 za Kazi Halmashauri ya Mji Korogwe July 06-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.

Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi
kwa nafasi zifuatazo:-

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – (NAFASI 5)

KAZI NA MAJUKUMU: –

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri;
  • Kupokea wageni na kuwasailisha shida zao, na kuwaelekeza sehemu
    wanapoweza kushughulikiwa;
  • Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miradi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati;
  • Kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote
    kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini;
  • Kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia
    kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi wake;
  • Kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazo husika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
  • Kutekeleza kazi zozote atakazo kuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutokakatia Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na.

Awe amepata mafunzo ya programu za Kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – (NAFASI 5)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (Incoming
    correspondence register);
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista
    (outgoing corresponding register);
  • Kusambaza majadala kwa watendaji (action officers);
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji;
  • Kutafuta kumbukumbu /nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji;
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (racks/filing cabinets); na
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (File tracking)

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu
Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS C

✅MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III – (NAFASI 8)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Katibu wa Kamati ya Mtaa;
  • Mtendaji Mkuu wa Mtaa;
  • Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na
    Halmashauri katika Mtaa;
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa;
  • Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria
    nyingine zinazotumika katika Mtaa;
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama;
  • Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa;
  • Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote;
  • Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

SIFA ZA MWOMBAJI
Mhitimu wa kidato cha Nne au Sita mwenye Cheti cha Mafunzo ya Astashahada katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Maendeleo ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Uchumi na Mipango kutoka vyuo vinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B

✅DEREVA DARAJA LA II – (NAFASI 4)

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
  • Kufanya usafi wa gari na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha kidato cha Nne (Form Four) na leseni Daraja E au C1 ya uendeshaji magari ambaye amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu
    walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Chetibcha mtihani wa Kidato cha IV na VI, –
  • Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
  • Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30bNovemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 18 Julai, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe
kwa: –

Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Korogwe,
1 Mtaa wa Halmashauri,
S.L.P. 615,
21268 Korogwe.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa
kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika
tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.