NAFASI 23 za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga July 09-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 23 za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga July 09-2024
NAFASI 23 za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga July 09-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Sumbawanga 09-07-2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha
tarehe 25/06/2024.
Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa
za kujaza nafasi zifuatazo:-
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (NAFASI 04)
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa/ kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika..
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya maitaji ya vifaa vya Ofisi.
SIFA ZA MWOMBAJI.
- Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI).
- Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katia Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na.
- Awe amepata mafunzo ya programu za Kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – C
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 04)
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuorodhosha barua zinazo zinazoingia masjala kwenye rejista.
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasis kwenye Rejista.
- Kusambaza majalada kwa watendaji.
- Kupokea majalada yanayorudi masijala toka kwa watendaji.
- Kutafuta kumbukumbu /nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji.
- Kurudisha majalada kwenye Shubaku/Kabati la majalada au mahali pengine yanapohifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi.
SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI).Awe amehitimu mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Masjala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa compyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – C
✅MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III (NAFASI 15)
KAZI NA MAJUKUMU
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mtaa.
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao kuwa mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala Bora katika Mtaa
- Kuratibu na kusimamia upangaji na utelekezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Mtaa
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Mtaa
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mkakati wa kuondoa njaa umaskini na kuongeza uzalishaji mali
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Mtaa
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Mtaa
- Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko ya migogoro ya Wananchi
- Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Mtaa na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
- Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wako
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne au Sita, Astashahada/Cheti NTA/LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Jamii kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali .
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mshahara ya Serikali ngazi ya Mshahara itakuwa TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma - Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
- “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 18 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi wa Manispaa ya
Sumbawanga,
S.L.P. 187,
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DONWLOAD PDF DOCUMENT
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NAFASI 23 za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga July 09-2024