RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 23 za Kazi Wilaya ya Mbozi July 17-2024

Filed in Ajira, Uncategorized by on 17/07/2024

NAFASI 23 za Kazi Wilaya ya Mbozi July 17-2024

NAFASI 23 za Kazi Wilaya ya Mbozi July 17-2024

NAFASI 23 za Kazi Wilaya ya Mbozi July 17-2024

NAFASI 23 za Kazi Wilaya ya Mbozi July 17-2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri Ya Wilaya ya Mbozi 17-07-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024.

Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma
maombi kwa kada tano (05) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuchapa barua,taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio ,miadi, wageni ,tarehe za vikao,safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya.kazi;
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika
    Idara/Kitengo/Sehemu husika;
  • Kukusanya ,kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali; na
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

SIFA ZA MWOMBAJI.
Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne au sita wenye Stashahada(Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili. Aidha ,wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile:Word,Excel ,Powerpoint ,internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS C

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II -NAFASI 2

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence register) ;
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista (outgoing
  • correspondence register) ;
  • Kusambaza, majalada kwa watendaji (action officers);
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji ;
  • Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji;
  • Kurudisha majalada kwenye kabati la majalada (racks/filing cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa;
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking) ; na
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha sita (Form VI) aliehitimu mafunzo ya Stashahada /Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali ,wenye ujuzi wa kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS C

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 10

MAJUKUMU YA KAZI

  • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya Kijiji;
  • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji;
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji;
  • Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalam waliopo katika Kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya Wananchi;
  • Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha kufaulu kidato cha Nne (IV) au cha sita (VI) na waliohitimu mafunzo ya Cheti (Astashahada) katika fani zifuatazo: Utawala, Uongozi na usimazi wa
Fedha, Sheria, Elimu ya Jamii, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Mshahara atalipwa kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGS B

✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 4

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
  • Kufanya matengenezo madogo ya gari;
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
  • Kufanya usafi wa gari; na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI.
Kuajiriwa mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Mshahara atalipwa kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGS B

✅MHUDUMU WA JIKONI -NAFASI 2

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kusafisha vyombo vya kupikia;
  • Kusafisha vyombo vya kulia chakula;
  • Kuwatayarishia wapishi/waandazi wa vifaa vya kazi;
  • Kusafisha maeneo ya kupikia;
  • Kuwasaidia waandazi wa wapishi; na
  • Kusafisha meza itumiwayo kwa kulia chakula.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne mwenye cheti cha mafunzo ya uhudumu jikoni kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Mshahara atalipwa kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGOS A

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipo kuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Adress) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
    kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita
    kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika Postgraduate/ Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards).
  • Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi nitarehe 30 Julai, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 3,
MBOZI

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretariet ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment
Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

Tags:

Comments are closed.