RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Kisarawe July 15-2024

Filed in Ajira by on 15/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Kisarawe July 15-2024

NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Kisarawe July 15-2024

NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Kisarawe July 15-2024

NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Kisarawe July 15-2024,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe amepokea kibali cha ajira mpya kutoka kwa katibu mkuu OR – Utumishi chenye Kumbu. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE 15-07-2024

Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada tatu (03) kama zilivyoanishwa kwa kuzingatia sifa tajwa:-

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (“Office Management
Secretary II”) NAFASI 5.

SIFA ZA MWOMBAJI.
kuajiriwa wa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili. aidha, wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II.

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu
    wanapoweza kushughulikiwa.
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika idara/kitengo/sehemu husika.
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

NGAZI YA MSAHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS C.

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (“Records Management Assistant II”)
NAFASI 5

SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (FORM IV) au cha Sita (FORM VI) aliyehitimu
mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kompyuta.

KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II.

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye rejista (incoming
    Correspondence register)
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing
    correspondence register)
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers)
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
    Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji:
  • Kurudisha majalada kwenye kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mshahara ya Serikali – TGS C

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 15.

SIFA ZA MWOMBAJI.
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne au Sita aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti (NTA Level 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI.

  • Kuwa Afisa Masuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani nanmsimamizi wa utawala bora katika kijiji.
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji.
  • Kuwa Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
  • Kutafsiri na kusimamia sera, sheria na taratibu:
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini
    na kuongeza uzalishaji mali.
  • Kuwa kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji:
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji
  • Kuwa mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika kijiji
  • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji.
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi na;
  • Atawajibika kwa mtendaji wa kata.

NGAZI YA MSAHAHARA: kwa kuzingatia Viwango vya Mishahara ya Serikali TGS B

MASHARTI YA UJUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Carriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • “Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
    kuzingatia sifa za kazi husika.
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).
  • Waombaji walisoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua kisheria.
  • Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 25 Julai, 2024

MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,
28 Barabara ya Bomani,
S.L.P 28001,
61401 Kisarawe,
KISARAWE.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani uii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.