RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Nyasa July 20-2024

Filed in Ajira by on 20/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Nyasa July 20-2024

NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Nyasa July 20-2024

NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Nyasa July 20-2024

NAFASI 25 za Kazi Wilaya ya Nyasa July 20-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa 21-07-2024,Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kupitia kibali cha ajira mpya chenye kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 chenye Kada za Mtendaji wa kijiji Daraja la III nafasi ishirini (20), Msaidizi wa kumbukumbu Daraja la II nafasi tano (5) Dereva Daraja la II nafasi nne (4), Mwandishi mwenndesha Ofisi nafasi tatu (3) na Msaidizi wa maendeleo ya jamii II (Community Development Assistant II) kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyasa anawatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa watanzania wote wenye sifa na kuleta maombi ya kazi kwa nafasi zilizoainishwa hapo chini.

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – NAFASI 5

MAJUKUMU YA KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista
  • Kusambaza majalada kwa watendaji Kupokea
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
    Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji.
  • Kurudisha majalada kwenye Shubaka/kabati la majalada au mahali pengine yanapohifadhiwa
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi

SIFA ZA MWOMBAJI:

Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliehitimu mafunzo ya
stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS C1 kwa mwezi.

✅MTENDAJI WA KIJIJI III – NAFASI 20

MAJUKUMU YA KAZI YA MTENDAJI WA KIJIJI III

  • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
  • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao,kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji
  • Kutafsiri na kusimamia Sera,Sheria na taratibu
  • Kuandaataarifa ya utekelezajiwa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchikatika kuandaa na kutekelezamikakati ya kuondoa njaa,umaskini na
    kuongeza uzalishaji mali
  • Kuwa Mwenyekiti wa kikao cha wataalam katika kijiji
  • Kusimamia,kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji
  • Mwenyekiti wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji
  • Kupokea,kusikiliza na kutatua migogora ya wananchi
  • Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo ndogo za kijiji na;
  • Kuwajibika kwa Mtendaji wa Kata.

SIFA ZA KITAALUMA KWA MWOMBAJI
Awe amefaulu Kidato cha nne (IV) au Kidato cha sita (VI )aliehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti au NTA level 5 katika mojawapo ya fani zifuatazo; Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka
vyuo vinachotambulika na Serikal.i

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS B1 kwa mwezi.

✅DEREVA DARAJA LA Il – NAFASI 4

MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA DARAJA II

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (log book)
  • Kufanya usafi wa gari.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne na Leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course)
yanayotolewa na Chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS B1 kwa mwezi

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI Il – NAFASI 3

MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI II

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaeleza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
  • Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika
    Idara/Kitengo/Sehemu husika;
  • Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha nne au sita wenye stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti NTA LEVEL 6 ya uhazili. Aidha wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingeleza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za Compyuta za ofisi kama vile Word, Exel, Powerpoint, Windows, Internet, E-mail na Publisher kutoka
chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS C1 kwa mwezi

✅MSAIDIZI WA MAENDELEO YA JAMII II – NAFASI 8

MAJUKUMU YA MSAIDIZI MAENDELEO II

  • Kusaidia kubuni na kupanga mipango ya Miradi ya Maendeleo katika eneo lake
  • Kusaidia uwezeshaji na upatikanaji na mafunzo kuhusu masuala ya Maendeleo katika eneo lake
  • Kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo
  • Kusaidia kutoa Elimu kuhusu kazi za kujitolea katika eneo lake.
  • Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya Jamii kila mwezi kwa uongozi wa Kijiji na kwa msimamizi wake wa kazi
  • Kusaidia kuunda Vikundi vya kijamii na vya Kimaendeleo
  • Kutambua na kuwezesha Kaya Maskini kuinua Uchumi wao kupitia fursa na Rasilimali zinazowazunguka.
  • Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Astashahada (Certificate) ya Maendeleo ya Jamii katika vyuo vya Maendeleo ya Jamii au vyuo vingine vinavyotambulika na Serikali katika moja wapo ya fani
zifuatazo; Maendeleo ya jamii(Community Development),Sayansi ya Jamii (Socialogy),Masomo ya Maendeleo (development studies),Mipango na usimamizi wa
Miradi(Project Planning and Management),Jinsia na maendeleo (Gender and Development),Maendeleo ya Vijijini ( Rural Development).Au Fani nyingine zinazofanana na
Maendeleo ya Jamii

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali – TGS B1 kwa mwezi

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi nabwanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na
    Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced
    Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from
    Respective Boards);
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
    HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
    Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Wakatakao kidhi Sifa zinazotakiwa ndio pekee watakaoitwa katika Usahili.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 02/08/2024

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
2 Barabara ya Nyerere
S.L.P. 90,
Mbamba Bay,
57582 Nyasa – Ruvuma

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira kupitia anwani
ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.