NAFASI 3 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Kondoa May 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 3 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Kondoa May 2024
NAFASI 3 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Kondoa May 2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Nafasi za Kazi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa May 20-2024, Nafasi za Ajira za Watendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa May 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuomba nafasi za kazi
iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na. FA 228/613/01/B/001 cha tarehe 22 Aprili 2023 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora.
1.0 MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III- (NAFASI 3)
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI)
- Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo; Sheria, Elimu ya
Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali
za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI
- Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kijiji;
- Katibu wa Kamati ya kijiji;
- Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Kijiji;
- Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Kijiji;
- Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika
katika Kijiji; - Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama;
- Msimamizi wa Mtekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na
- Umasikini katika Kijiji;
- Kusimamia Ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa
kodi; na - Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
NGAZI YA MSHAHARA
Ngazi ya mshahara ni TGS B.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili;
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika
kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao
na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia
kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, -Cheti cha mtihani wa
Kidato cha IV na VI, -Computer Certificate, -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates
from respective boards) - “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha
nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi
wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC.
45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 02 Juni, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
KUTUMA MAOMBI BONYEZA HAPA
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa More Details |
2024-06-02 Login to Apply |
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Ajira za Watendaji wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, NAFASI 3 za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Kondoa May 2024, Nafasi za Ajira za Watendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa May 2024., Nafasi za Kazi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa May 20-2024