NAFASI 31 za Kazi Wilaya ya Muheza July 22-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 31 za Kazi Wilaya ya Muheza July 22-2024
NAFASI 31 za Kazi Wilaya ya Muheza July 22-2024,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza amepokea kibali cha Ajira
mbadala chenye Kumbukumbu Na.FA.228/613/01/D/020 cha tarehe 21/06/2024, na kibali cha Ajira mpya chenye Kubukumbu.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024.
Kwa Ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 2
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne au sita mwenye stashahada (diploma ya
uhazili au cheti cha NTA LEVEL 6 ya uhazili. Aidha awe amefaulu somo la hatimkato ya Kiswahili na kingereza maneno 100 kwa dakika 1 na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: word, Excel, Powerpoint, Internet, Email na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri;
- Kupokea wageni na kuwasailisha shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
- Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miradi, wageni, tarehe za vikao, safari
za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi
anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati; - Kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini;
- Kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi wake;
- Kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazo husika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
- Kutekeleza kazi zozote atakazo kuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C
✅💪MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – (NAFASI 24)
SIFA ZA MWOMBAJI
Mhitimu wa kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) mwenye Cheti cha Mafunzo ya Stashahada katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Maendeleo ya Jamii, Usimamizi wa Fedha,
Uchumi na Mipango kutoka vyuo vinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
- Katibu wa Kamati ya Mtaa;
- Mtendaji Mkuu wa Mtaa;
- Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa;
- Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa;
- Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa;
- Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama;
- Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa;
- Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote;
- Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B
✅DEREVA DARAJA LA II – (NAFASI 5)
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha kidato cha Nne (Form Four) na leseni Daraja E au C1 ya uendeshaji magari ambaye amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
- Kufanya usafi wa gari na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya
taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma - Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza
(DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. - Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa
zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V)
yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa
na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa
wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
- Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE). - Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 31 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ,
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza,
4 Barabara ya Bomani,
S.L.P. 20,
21402 MUHEZA-TANGA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.