RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 36 za Kazi Halmashauri ya Mji kibaha July 16-2024

Filed in Ajira by on 16/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 36 za Kazi Halmashauri ya Mji kibaha July 16-2024

NAFASI 36 za Kazi Halmashauri ya Mji kibaha July 16-2024

NAFASI 36 za Kazi Halmashauri ya Mji kibaha July 16-2024

NAFASI 36 za Kazi Halmashauri ya Mji kibaha July 16-2024,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha amepokea kibali cha Ajira mpya kutoka kwa
Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MJI KIBAHA 16-07-2024

Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada nne (04) kama zilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa: –

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (“Office Management Secretary II”) NAFASI 04

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika idara/ kitengo/sehemu husika.
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama
vile Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS C

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (“Records Management Assistant II”)NAFASI 05

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence regisster)
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi kwenye rejista (outgoing
    correspondence register)
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers)
  • Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji
  • Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/mafaili yanayohitajika na watendaji.
  • Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa Kumbukumbu/nyaraka.
  • Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification and Boxing) kwaajili ya matumizi ya ofisi.
  • Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (File Racks/Cabinets) katika
    masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
  • Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
  • Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliehitimu
mafunzo ya stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Masijala kutoka
vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS C

✅MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III (“MTAA Executive”) NAFASI – 20

KAZI NA MAJUKUMU

  • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mtaa
  • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Mtaa,
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo katika Mtaa
  • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Mtaa
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
  • Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
  • Mwenyekiti wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Mtaa
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Mtaa
  • Kuwa Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika Mtaa
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi
  • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo kwenye Mtaa na;
  • Kuwajibika kwa Mtendaji wa Kata.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada/Cheti au NTA level 5 katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala,
Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya
Sanaa kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali- TGS B

✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 07

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.Kufanya kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari na
  • Kufanya Usafi wa Gari.
  • Kufanya kazi nyingine kadri atavyoelekezwa na msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na elimu ya kidato cha Nne (IV) na kupata cheti cha mtihani wa kidato cha
Nne (IV) Awe na leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia
kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (01) bila kusababisha ajali. Awe
amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS B

MASHARTI YAJUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya
    taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Carriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • “Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne
    na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao
    na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi
    wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na.
    CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional
    Certificate from Respective Boards).
  • Waombaji walisoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka
    husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 28 Julai, 2024

MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja
na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:

MKURUGENZI,

HALMASHAURI YA MJI KIBAHA,

S.L.P 30112

KIBAHA.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti
ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

DONWLOAD PDF DOCUMENT

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.