RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 38 za Madaktari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe July 2024

Filed in Ajira by on 30/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 38 za Madaktari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe July 2024

NAFASI 38 za Madaktari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe July 2024

NAFASI 38 za Madaktari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe July 2024

NAFASI 38 za Madaktari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe July 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe anatangaza nafasi za ajira ya mkataba kwa yeyote atakaekuwa na sifa stahiki katika kada husika.

NAFASI ZINAZOTANGAZWA NI KAMA ZIFUATAZO;

✅DAKTARI DARAJA LA PILI (NAFASI 1)

SIFA ZA DAKTARI DARAJA LA PILI
Awe mwenye shahada ya udaktari kutoka chuo kikuu kinachotambulika na serikali waliohitimu mafunzo ya mazoezi katika kazi (internalship) yaliyoidhinishwa na baraza la madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika) na kusajiriwa kisheria na baraza hilo

MAJUKUMU YA DAKTARI DARAJA LA PILI

  • Kufanya shughuli zote za matibabu Hospitalini zinazohusiana na magonjwa ya kawaida, magonjwa ya watoto,magonjwa ya akina mama na upasuaji wa kawaida na dharura
  • Kufanya kazi zote za kinga na afya ya jamii na kubuni mikakati ya kupambana na magonjwa yanayoambukizwa
  • Kusimamia watumishi wodini na sehemu nyingine za kazi
  • Kusimamia watumishi wodini na sehemu nyingine za kazi 5. Kutoa ushauri nasaha kwa wagonjwa na jamii kwa ujumla
  • Kufundisha wanafunzi wa vyuo vya uganga
  • Kufundisha na kuwaendeleza kitaaluma watumishi walioko kwenye hospitali 8. Kufanya utafiti kuhusu magonjwa na kueneza matokeo ya utafiti kwa jamii
  • Kupanga,kufuatilia na kutathimini utoaji wa huduma za afya
  • Kufanya kazi nyingine atakazokupangiwa na mkuu wake wa kazi

MUUGUZI DARAJA LA PILI (EN) (NAFASI 24)

SIFA ZA DAKTARI DARAJA LA PILI
Awe mwenye cheti cha uuguzi cha miaka miwili kutokakwa chuo kinachotambuliwa na serikali na kuandikishwa (enrolled) na baraza la wauguzi wa wakunga Tanzania.

MAJUKUMU ZA DAKTARI DARAJA LA PILI

  • Kufanya kazi za kiuguzi kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu na sehemu zote zinapotolewa huduma za afya
  • Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya kazi
  • Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji
  • Kutoa huduma kwa wagojwa majumbani
  • Kutoa ushauri nasaha
  • Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango
  • Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya
  • Kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi
  • Kufanya kazi nyingine atakazokupangia mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu,uzoefu na ujuzi wake
NAFASI 38 za Madaktari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe July 2024

NAFASI 38 za Madaktari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe July 2024

MHUDUMU WA AFYA (NAFASI 7)

SIFA ZA MHUDUMU WA AFYA
Awe mhitimu wa kidato cha nne aliepata mafunzo ya mwaka mmoja katika fanio ya afya na akiwa na cheti cha ADDO atapewa nafasi ya kipaumbele

MAJUKUMU YA MHUDUMU WA AFYA

  • Kufanya usafi wa vifaa vya kazi, usafi wa wodi na mazingira
  • Kusaidia wagonjwa wenye ulemavu na wasiojiweza katika kwenda haja na kuoga
  • Kumsaidia kumlisha mgonjwa asiyejiweza
  • Kuchukua nguo za wagonjwa kuzipeleka kwenda kufuliwa
  • Kuchukua sampuli za mgonjwa kwaajili ya vipimo vya maabara na kufuatilia majibu
  • Kutayarisha vifaa kwaajili ya kusafisha na kufunga majeraha
  • Kufuatilia mahitaji ya dawa kwa wagonjwa kutoka hifadhi ya dawa
  • Kufanya shughuli nyingine atakazopangiwa na kiongozi wake wa kazi

✅MTEKNOLOGIA MAABARA DARAJA LA PILI (NAFASI 2)

SIFA MTEKNOLOGIA MAABARA DARAJA LA PILI
Awe mwenye stashahada katika fani ya uteknolojia maabara katika chuo kinachotambulika na serikali na ambao wamesajiliwa na baraza la maabara Tanzania na wenye leseni hai

MAJUKUMU MTEKNOLOGIA MAABARA DARAJA LA PILI

  • Kupima sampuli zinazotolewa maabara
  • Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa maabara ngazi ya juu
  • Kufanya kazi za ukaguzi wa maabara, vitendanishi,vifaa, kemikali na hifadhi ya kemikali
  • Kuweka kumbukumbu za maabara ambazozimepatikana wakati wa uchunguzi 5. Kufundisha watumishi waliochini yake
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu,uzoefu na ujuzi wake

MTOA DAWA USINGIZI (NAFASI 4)

SIFA ZA MTOA DAWA USINGIZI
Awe mwenye cheti cha uuguzi cha miaka miwili kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali au mwenye cheti cha tabibu aliyesomea utoaji dawa za usingizi kwa muda usiopungua miezi sita au

MAJUKUMU YA MTOA DAWA USINGIZI

  • Kumuandaa mgonjwa na kumuwekea mpango kabla ya upasuaji
  • Kuandaa na kutoa aina nzuri ya dawa ya usingizi kwa upasuaji uliopangwa kwa mgojwa husika
  • Kujengea watu uwezo namna ya kutunza vifaa vya kutolea dawa za usingizi pamoja na kutoa oxygeni
  • Kuyakabili maumivu kabla na baada ya upasuaji
  • Kupanga nakutoa huduma za M-koba za kutoa dawa za usingizi
  • Kutoa elimu juu utunzaji wa kumbukumbuza huduma zilizotolewa kwa mgonjwa
  • Kufanya majukumu mengine utakayopangiwa na mganga mfawidhi

MAJUKUMU YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 18-45.
  • Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Waombaji wote waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza “detailed cv yenye anuani na namba za simu za kuaminika.
  • Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili au kingereza.
  • Waombaji wote kwenye barua za maombi waandike namba za simu za uhakika kwaajiliya mawasiliano.

Maombi yote yatumwe kupitia anuani ya posta kama ifuatavyo;
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Songwe.
S.L.P.77
Mkwajuni -Songwe
Mwisho wa kupokea maombi ni 7/8/2024 saa 9:30 alasiri

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.