NAFASI 390 za Walimu wa Kiingereza Ajira za Walimu 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 390 za Walimu wa Kiingereza Ajira za Walimu 2024
NAFASI 390 za Walimu wa Kiingereza Ajira za Walimu 2024,Ajira Mpya za Walimu 2024/2025, Nafasi za Walimu wa Awali Ajira za Walimu 2024.
MWALIMU DARAJA LA III B – KIINGEREZA (ENGLISH) NAFASI 390
(Songwe 11, Iringa 11, Katavi 15, Simiyu 41, Mara 22, Kigoma 15, Rukwa 17,
Kagera 13, Ruvuma 14, Dar es Salaam 5, Pwani 4, Geita 18, Singida 16, Tanga 32,
Manyara 7, Tabora 12, Shinyanga 17, Njombe 3, Mtwara 27, Dodoma 6, Morogoro 46, Kilimanjaro 23, Mbeya 10 na Lindi 5)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na
Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa; - Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
- Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
- Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
- Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
- Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
- Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
- Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Kiingereza kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulIka na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGTS- C.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE WA AJIRA ZA WALIMU 2024
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.Waombaji wa nafasi za Mwalimu Daraja la III B na Mwalimu Daraja la III C
- wahakikishe wanambatisha HATI YA MATOKEO (ACADEMIC TRANSCRIPT) katika mfumo wa “Ajira Portal” kwa ajii ya utambuzi wa masomo ya kufundishia.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi nabwanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionaonkwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha I na Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards).
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 02 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamojana vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (RecruitmentPortal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: Ajira Mpya za Walimu 2024/2025, NAFASI 390 za Walimu wa Kiingereza Ajira za Walimu 2024, Nafasi za Walimu wa Awali Ajira za Walimu 2024.