RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 4 za Kazi Wizara ya Afya March 2024

Filed in Ajira, Michezo by on 08/03/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 4 za Kazi Wizara ya Afya March 2024

NAFASI 4 za Kazi Wizara ya Afya March 2024,Wizara Ya Afya Ajira 2024, ajira.moh.go.tz login, Waliochaguliwa Ajira wizara Ya Afya,ajira.moh.go.tz login password, Wizara ya Afya Tanzania, Wizara ya Afya contacts.

NAFASI 4 za Kazi Wizara ya Afya March 2024

NAFASI 4 za Kazi Wizara ya Afya March 2024,Wizara Ya Afya Ajira 2024, ajira.moh.go.tz login, Waliochaguliwa Ajira wizara Ya Afya,ajira.moh.go.tz login password, Wizara ya Afya Tanzania, Wizara ya Afya contacts.

Wizara ya Afya inalo jukumu la kusimamia Kada za Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalamu wa Afya Shirikishi nchini kupitia Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) lililoundwa chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Udaktari, Udaktari wa Meno na Wataalamu wa Afya Shirikishi (Sura Na. 152).

Lengo kuu la Baraza ni kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma bora na salama kutoka kwa Wanataaluma.

Katika kuimarisha na kuboresha huduma za Afya nchini, Wizara inatarajia kuajiri Afisa Habari mmoja (01) na Watoa Huduma kwa Wateja (Call Centre Agents Watatu (03) kwa mkataba wa miezi Kumi na Moja (11).

Sifa na Majukumu kwa kila kada zimeainishwa kama ifuatavyo: –

NA KADA ZINAZOHITAJIKA
1.

Afisa Habari Daraja la II – (Nafasi 1)

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Kuajiriwa mwenye Shahada ya uandishi wa habari au sifa nyingine inayofanana na hiyo kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali na uzoefu usiopungua miaka mitatu (3).

KAZI NA MAJUKUMU:

  • Afisa Habari Daraja la II atawajibika na mahitaji yote ya kitaaluma yanayohusiana na kuharakisha mawasiliano baina ya Baraza na Wanataaluma/wateja wa Baraza.
  • Kukuza Sera, kazi na Program za Baraza.
  • Kukusanya na kuandika habari.
  • Kuandaa na kutekeleza mkakati wa mawasiliano ya Baraza na Jamii.
  • Kufanya mazungumzo na wananchi pamoja na vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Baraza.
  • Kutoa na kusambaza nyaraka kama vile vipeperushi, makala na majarida.
  • Kuratibu taarifa kwa Waandishi wa Habari.
  • Kupiga picha za matukio yote yanayohusu Baraza na kuhudumia Maktaba na marejeo.
  • Kukusanya takwimu mbalimbali.
    ix. Kutekeleza majukumu mengine utakayopangiwa na Mwajiri.

Watoa Huduma (Call Center Agents) – (Nafasi 03)

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Kuajiriwa mwenye Shahada ya Mahusiano ya Umma (Public Relations), Mawasiliano ya Umma (Mass Communication), Utawala, Usimamizi wa Rasilimali watu, au sifa nyingine zinazofanana na hizo kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.

NAFASI 4 za Kazi Wizara ya Afya March 2024,Wizara Ya Afya Ajira 2024, ajira.moh.go.tz login, Waliochaguliwa Ajira wizara Ya Afya,ajira.moh.go.tz login password, Wizara ya Afya Tanzania, Wizara ya Afya contacts.KAZI NA MAJUKUMU:

  • Kupokea simu za Wanataaluma na wateja wengine wa Baraza na kutoa majibu sahihi ya kuridhisha, kwa wakati;
  • Kutoa usaidizi kwa Wanataaluma na Wateja wa Baraza kupitia simu na mitandao;
  • Kutatua matatizo yaliyo ndani ya uwezo wake na kuyashughulikia kutoka kwa wateja wanaopiga simu;
  • Kuwasilisha kwa rufaa matatizo yaliyo juu ya uwezo wake kwa wasimamizi wake, na kutoa mrejesho kwa Wanataaluma baada ya kupatiwa ufumbuzi;
  • Kupiga simu kwa Wanataaluma na wateja wengine wa Baraza na kuwafahamisha kuhusu masuala mbalimbali ya Baraza la Madaktari;
  • Kuwaongoza Wanataaluma wanaopiga simu juu ya namna ya kutumia mfumo wa TEHAMA wa Baraza la Madaktari;
  • Kutunza rejista ya simu;
  • Kupitia akaunti za Wanataaluma wanaopiga simu katika mfumo wa TEHAMA na kuelimisha, kutoa ushauri na maelekezo mengine kuhusu masuala yatakayobanika;
  • Kutoa mapendekezo kwa msimamizi wake juu ya masuala yanayohusiana na kituo cha huduma kwa wateja cha Baraza;
  • Kushirikiana na wataalamu wengine wa vituo vya huduma kwa wateja ili kuboresha huduma;
  • Kufanya kazi nyingine yoyote kama atakavyoagizwa na msimamizi wake;
  • Kuingiza taarifa kwenye mfumo wa ukusanyaji taarifa;
  • Kufanya ufuatiliaji wa hoja na malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi; na
  • Kutekeleza majukumu mengine utakayopangiwa na Mwajiri.
    Maelekezo ya kuzingatiwa kwa waombaji:

Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi Dodoma (Makao Makuu ya Baraza).

Nakala za vyeti vyote zithibitishwe na Mahakama au Wakili.

SIFA ZA UJUMLA KWA MWOMBAJI:

  • Awe raia wa Tanzania;
  • Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 50;
  • Asiwe mwajiriwa wa Serikali au mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;
    na
  • Awe na sifa na weledi kwa Mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba. 1 wa mwaka 2009.

Maombi yote yaambatishwe na; –

  • Nakala ya Cheti cha kuzaliwa;
  • Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne/Sita na Stashahada/Shahada kulingana na Kada iliyoainishwa;
  • Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje waambatishe cheti cha Ithibati kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA);
  • Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts).
  • Aidha, waliosoma vyuo vya nje ya nchi, waambatishe cheti cha Ithibati kutoka TCU;
  • Wasifu (CV);
  • Picha ndogo (Passport size) mbili za hivi karibuni;
  • Nakala ya Kitambulisho cha uraia (NIDA)/Namba ya Utambulisho ya NIDA; na
  • Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na Cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa Viapo na kusajiliwa na Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI:

  • Muda wa kutuma maombi haya ni ndani ya wiki mbili (2) kuanzia tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili.
  • Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Wizara unaopatika kupitia tovuti ajira.moh.go.tz
  • Waombaji wote mnakumbushwa kuwa makini mnapowasilisha maombi kuhakikisha umejaza vizuri vipengele vyote vinavyotakiwa kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kuambatisha nyaraka zote zinazohitajika.

Tangazo limetolewa na:
KATIBU MKUU
WIZARA YA AFYA
S.L.P 743 DODOMA
08/03/2024

NAFASI 4 za Kazi Wizara ya Afya March 2024 Download PDF

Wizara ya Afya Tanzania address, Wizara ya Afya Zanzibar, Anwani ya katibu mkuu wizara ya afya dodoma, NAFASI za KAZI Wizara ya Afya 2024, Ajira za afya sekta binafsi,TAMISEMI Ajira za Afya.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , , , , ,

Comments are closed.