KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

NAFASI 4 za Mtendaji wa Kijiji Kutoka Wilaya Ya Same 21-05-2024

Filed in Ajira by on 21/05/2024 0 Comments

NAFASI 4 za Mtendaji wa Kijiji Kutoka Wilaya Ya Same 21-05-2024

NAFASI 4 za Mtendaji wa Kijiji Kutoka Wilaya Ya Same 21-05-2024, Nafasi za Kazi Kutoka Wilaya Ya Same 21-05-2024, Ajira Mpya Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Same Leo May 2024, Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Same Leo tarehe 21-2024,TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME 21-05-2024.

NAFASI 4 za Mtendaji wa Kijiji Kutoka Wilaya Ya Same 21-05-2024

NAFASI 4 za Mtendaji wa Kijiji Kutoka Wilaya Ya Same 21-05-2024, Nafasi za Kazi Kutoka Wilaya Ya Same 21-05-2024, Ajira Mpya Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Same Leo May 2024, Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Same Leo tarehe 21-2024,TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME 21-05-2024.

Kufuatia Halmashauri ya Wilaya ya Same kupata kibali cha ajira mbadala chenye Kumb.Na.FA.228/613/01/A/055 cha Tarehe 8 Februari 2024 na kibali chenye Kumb.Na.FA.228/613/01/B/048 cha tarehe 15 Machi 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu ajira mpya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same anatangaza nafasi
za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kama zilivyoorodheshwa katika tangazo hili:-

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI NNE (4)

SIFA ZA MWOMBAJI

 • Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha nne/sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) Katika moja wapo ya fani zifuatazo: Utawala,
  Sheria, Elimu ya Jamii, usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI

 • Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
 • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao,kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji.
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Mendeleo ya kijiji.
 • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya kijiji
 • Kutafsiri na kusimamia sera,sheria na taratibu
 • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
 • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika kijiji.
 • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
 • Mwenyekiti wa kikao cha wataalaamu waliopo katika kijiji
 • Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
 • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji na atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali TGS B

MASHARTI KWA JUMLA

 • Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
 • Waombaji wenye ulemavu wnahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
 • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua
  pepe (E- mail address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
 • Provisional/Testimonials/Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha nne na sita (form IV na VI result slip) HAVITAKUBALIWA.
 • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
 • Wombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
 • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe iapasavyo.
 • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na Wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyokatika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
 • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbali mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
 • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA)
 • Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahausika watachukuliwa hatua za kisheria
 • Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza

MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME
SLP.138
SAME.

Maombi yote Ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https:portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Ijumaa, tarehe 03 JUNI, 2024.

NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME 21-05-2024 DONWLOAD PDF DOCUMENT

Historia

HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME

HISTORIA YA WILAYA YA SAME.

UTANGULIZI

Halmashauri ya Wilaya ya Same ilianzishwa rasmi kwa Sheria ya Bunge Sura ya 287 (Mamlaka za Wilaya) ya Sheria za Tanzania na ilianza kutekeleza majukumu yake tarehe 01 Januari 1984. Aidha Halmashauri ina Idara 13 na vitengo 6 ambavyo vinatekeleza majukumu mbalimbali kama ambavyo imeanishwa hapo chini:-

1.0  IDARA YA AFYA  

1.1 Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)

Asilimia 30.6 ya kaya za Wilaya ya Same zimejiunga na CHF. Kwa Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Same ni ya 3 Kati ya Wilaya saba za Mkoa.

1.1.1 Mipango/Mikakati Iliyopo kufikisha 80%

 1. Kuhakikisha     walengwa wanaopata Fedha kupitia mpango wa Kaya maskini-TASAF wanajiunga     na mfuko wa CHF
 2. Kutumia     wanafunzi wa shule wakiwa kwenye makundi ya watu sita kujiunga na CHF kwa     mfano Same Sekondari.
 3. Bodi ya     Afya ya Wilaya kufanya ziara ya uhamasishaji kwa kamati za vituo vya Afya     kujiunga na CHF.
 4. Kamati za     Afya za vituo kufanya uhamasishaji kwa jamii kupia mikutano ya vijiji na     CHF kuwa Agenda ya kudumu kwenye vikao vya vijiji.

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *