RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 488 za Walimu wa Kemia Ajira za Walimu 2024

Filed in Ajira by on 21/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 488 za Walimu wa Kemia Ajira za Walimu 2024

NAFASI 488 za Walimu wa Kemia Ajira za Walimu 2024,Ajira Mpya za Walimu 2024/2025, Nafasi za Walimu wa Awali Ajira za Walimu 2024.

NAFASI 488 za Walimu wa Kemia Ajira za Walimu 2024

NAFASI 488 za Walimu wa Kemia Ajira za Walimu 2024,Ajira Mpya za Walimu 2024/2025, Nafasi za Walimu wa Awali Ajira za Walimu 2024.

MWALIMU DARAJA LA III B – KEMIA (CHEMISTRY) NAFASI 488
(Mtwara 17, Njombe 12, Tanga 26, Singida 20, Kilimanjaro 23, Morogoro 31, Mbeya 23, Lindi 18, Kagera 22, Mwanza 35, Arusha 24, Ruvuma 14, Katavi 3, Rukwa 16, Songwe 15, Iringa 15, Dar es Salaam 9, Dodoma 9, Shinyanga 10, Manyara 22, Mara 19, Tabora 16, Kigoma 30, Simiyu 21, Geita 25 na Pwani 13).

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na
    Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
  • Kufundisha, kufanya Tathimini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za shule; na
  • Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Kemia kutoka Vyuo vya
Ualimu vinavyotambulika na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGTS- C.

JINSI YA KUJISAJILI NA KUTUMA MAOMBI BONYEZA HAPA

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE WA AJIRA ZA WALIMU 2024

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.Waombaji wa nafasi za Mwalimu Daraja la III B na Mwalimu Daraja la III C
  • wahakikishe wanambatisha HATI  YA MATOKEO (ACADEMIC TRANSCRIPT) katika mfumo wa “Ajira Portal” kwa ajii ya utambuzi wa masomo ya kufundishia.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi nabwanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionaonkwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  •  Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. 
  • Cheti cha mtihani wa kidato cha I  na   Computer Certificate
  •  Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards).
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo
    katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 02 Agosti, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamojana vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (RecruitmentPortal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , ,

Comments are closed.