NAFASI 50 za wakusanya taarifa za Majengo Manispaa ya Kigamboni July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 50 za wakusanya taarifa za Majengo Manispaa ya Kigamboni July 2024
NAFASI 50 za wakusanya taarifa za Majengo Manispaa ya Kigamboni July 2024, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni anapenda kuwatangazia nafasi 50 (Hamsini) za ajira ya muda mfupi ya kazi ya kukusanya taarifa za Majengo kwa Kata na Mitaa yote ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Zoezi hili linatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku 90 (miezi mitatu) ikiwa ni utekelezaji wa uhuishaji wa kanzidata ya taarifa za majengo kwa lengo la kukusanya kodi ya majengo kama ilivyoainishwa kwenye Sheria ya Fedha za Serikali ya Mitaa sura 290, 2019 na marekebisho yake ya mwaka 2023.
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe raia wa Tanzania na anayeishi katika Wilaya ya Kigamboni;
- Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 35:
- Awe amehitimu angalau Kidato cha nne;
- Awe na uwezo wa kusoma na kuelewa vema lugha ya Kiingereza:
- Awe na namba au kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na NIDA;
- Awe mwenye afya njema atakayeweza kuzunguka mtaani kukusanya taarifa;
- Awe na simu janja yenye mfumo wa uendeshaji wa Android yenye uwezo wa kutunza chaji kwa masaa 12 na aweze kuitumia;
- Awe na anuani ya barua pepe (email address) na nywila (password) inayofanya kazi;
- Awe na uwezo wa kusoma Ramani za Mitaa;
KAZI NA MAJUKUMU
- Kukusanya na kuingiza taarifa za majengo kwa usahihi katika mfumo wa ODK;
- Kukusanya taarifa za wamiliki wa majengo,
- Kutumia mfumo wa ODK utakaowekwa katika simu janja kwa kukusanya taarifa za majengo kieletroniki:
- Kupiga picha ya pande tatu (3D) majengo kwa kutumia simu janja na kuhifadhi katika mfumo wa ukusanyaji taarifa:
MALIPO
Kazi itafanyika kwa muda wa siku 90 kuanzia tarehe 06 Agosti, 2024 kwa malipo ya TShs 7,000.00 kwa siku.
MAOMBI YAAMBATISHWE NA
- Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne na kuendelea:
- Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa;
- Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au namba ya Kitambulisho cha Taifa;
- Picha mbili za hivi karibuni (Passport size photograph);
JINSI YA KUTUMA MAOMBI YA KAZI
Barua zote za maombi ya kazi zielekezwe kwa:
Mkurugenzi wa Manispaa
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
S.L.P 36009
2 Barabara ya Mashujaa
17882 KIGAMBONI
Barua zote za maombi ya kazi zipitishwe na Mtendaji wa Mtaa anapoishi mwombaji:
Upande wa mbele wa Bahasha ya maombi, eneo la juu kulia landikwe: Kumb. Na. DA.215/386/02/24;
Barua za maombi zipelekwe katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata unayoomba;
Mwisho wa kutumia maombi ya kazi ni siku ya Jumatano tarehe 31 Julai 2024, saa 9:00 Alasiri.
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NAFASI 50 za wakusanya taarifa za Majengo Manispaa ya Kigamboni July 2024