NAFASI 56 za Kazi Hospitali ya Lutheran Kilindi July 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 56 za Kazi Hospitali ya Lutheran Kilindi July 2024
NAFASI 56 za Kazi Hospitali ya Lutheran Kilindi July 2024,Mkurugenzi wa Hospitali ya Kilutheri ya Kilindi inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anatangaza nafasi za kazi 56 za Kada za Afya kama ifuatavyo:
MAJINA 33990 ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi July 2024
✅DAKTARI DARAJA LA II (NAFASI 5)
- Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Waombaji wawe wamemaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
✅DAKTARI MSAIDIZI DARAJA LA II (NAFASI 4)
- Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya juu ya Tiba kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali walio na Leseni ya kufanya kazi kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council Tanganyika).
✅AFISA MUUGUZI DARAJA LA II (NAFASI 2)
- Waombaji wawe na Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo kwa vitendo (Internship) ya mwaka mmoja ambao wamesajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurses and Midwifery Council).
✅TABIBU DARAJA LA II (NAFASI 6)
- Waombaji wawe na Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
✅TABIBU WA MENO DARAJA LA II (NAFASI 2)
- Waombaji wawe na Stashahada ya Tabibu Meno (Diploma in Clinical Dentistry) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
✅MUUGUZI DARAJA LA II (NAFASI 30)
- Waombaji wawe na cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).
✅MTEKNOLOJIA WA MACHO DARAJA LA II (TECHNOLOGIST – OPTOMETRIST) (NAFASI 1)
- Kuajiriwa wenye Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Macho kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali, ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalam Macho.
✅MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (DAWA) DARAJA II (NAFASI 1)
- Waombaji wawe na Cheti cha kidato cha nne, Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Dawa kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).
✅MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (MAABARA) (NAFASI 1)
- Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Certificate in Health Laboratory Science) kwa muda wa miaka miwili kutoka
Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la
Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).
NAFASI 56 za Kazi Hospitali ya Lutheran Kilindi July 2024
✅MTEKNOLOJIA (MIONZI) DARAJA II (NAFASI 1)
- Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Mionzi (Diploma in Radiology/Radiography) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Waombaji wawe wamesajiliwa na Baraza la
Wataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology and Imaging
Professionals Council).
✅AFISA AFYA MAZINGIRA MSAIDIZI DARAJA LA II (NAFASI 1)
- Waombaji wawe na Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira ya miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Baraza la
Wataalamu wa Afya ya Mazingira (The Environmental Health Practitioners’ Registration Council).
✅DOBI (NAFASI 1)
- Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika Vyuo vinavyotambulika na Serikali.
✅DEREVA (NAFASI 1)
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV), Leseni ya udereva Daraja E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanya kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI
- Awe raia wa Tanzania;
- Awe na umri usiozidi miaka 45;
- Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato cha Nne, Sita, Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au Leseni hai
ya kufanya kazi ya taaluma husika); - Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;
- Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma;
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed
C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika. - Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIN); na
- Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yatumwe ndani ya wiki moja tangu tarehe ya kutoka kwa tangazo hili (mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 27/07/2024.
Barua ya maombi ielekezwe kwa anuani,
Mkurugenzi wa Hospitali ya Kilutheri Kilindi,
S. L. P 92 SONGE- KILINDI
Maombi yote yatumwe kwenye Email: kilindilutheranhospital@yahoo.com.
Kwa mawasiliano; +255655 379 883 / +255712 630 405
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NAFASI 56 za Kazi Hospitali ya Lutheran Kilindi July 2024