KUITWA KWENYE USAILI NEC 2024 TAZAMA HAPA


RATIBA KAMILI NA MAKUNDI YA EURO 2024 TAZAMA HAPA


WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2024 TAZAMA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA

NAFASI 8 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya Ya Geita 15-05-2024

Filed in Ajira, Michezo by on 15/05/2024 0 Comments

NAFASI 8 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya Ya Geita 15-05-2024

NAFASI 8 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya Ya Geita 15-05-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita May 15-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita May 2024,TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA 15-05-2024.

NAFASI 8 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya Ya Geita 15-05-2024

NAFASI 8 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya Ya Geita 15-05-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita May 15-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita May 2024,TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA 15-05-2024.

Halmashauri ya Wilaya ya Geita imepokea kibali cha Ajira chenye Kumb.
Na.FA.228/613/01/B/081 cha terehe 22 Aprili, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu ajira mbadala, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita anatangaza nafasi za kazi na
anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kama
zilivyoorodheshwa katika Tangazo hili.

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (NAFASI 8)

SIFA ZA MUOMBAJI

 • Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI)
 • Awe na Astashahada/ Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Rasilimali watu, Sheria, Maendeleo ya Jamii, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha au Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
 • JINSI ya Kutuma Maombi Ajira za Jeshi la Polisi Tanzania

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI

 • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
 • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na
 • Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaii wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
 • Kuratibu Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
 • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na taratibu za uendeshaji wa Serikali ya Kijiji.
 • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na
  kuongeza uzalishaji mali.
 • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.
 • Kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote katika Kijiji.
 • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

MSHAHARA

 • Kwa kuzingatia ngazi ya Mishahara ya Serikali, yaani TGS B kwa mwezi.

MASHARTI KWA UJUMLA

 • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
 • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma.
 • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
 • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
  katika Kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
 • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees)
  watatu wenye kuaminika.
 • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma,maelezo,nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha nne,
  Kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzobmbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
 • “Testimonials, Provisional Results, Statement of Result” na hati za matokeo kidato cha Nne na Sita (form IV na VI Result Slips) HAVITAKUBALIWA.
 • Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimekaguliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (NECTA, NACTE na TCU)
 • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana Kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
 • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
 • Waombaji kazi ambao tayari ni Waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia Maelezo yaliyo katika
  Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa Tarehe 30 Novemba, 2010.
 • Uwasilishwaji wa taarifa za sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua Stahiki za Kisheria.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 27/05/2024.

MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliosainiwa
pamoja na vyeti vya Elimu.

Aidha, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Geita,
S.L.P 139,
GEITA.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa
ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz/ Anuani
hii pia inapaikana kwenye Tovuti ya Sekretariet ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa Recruitment Portal”).

Maombi yatakayo wasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na;
Karia R. Magaro
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI GEITA DC DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

NAFASI 8 za Watendaji wa Vijiji Kutoka Wilaya Ya Geita 15-05-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita May 15-2024, Ajira za Watendaji wa Vijiji Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita May 2024,TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA 15-05-2024.

Historia ya Wilaya ya Geita

Wilaya ya Geita ni moja ya wilaya 5 zinazounda mkoa wa Geita. Ilipata hadhi ya kuwa wilaya mwaka 1962.Kipindi hicho iliitwa Geita province.Wilaya ya Geita ipo kati ya mita 1,100 hadi 1,300 kutoka usawa wa bahari.Pia ipo katika latitudi 208 hadi 3028 kusini mwa mstari wa ikweta na longitudi 32045 na 370 mashariki mwa mstari wa Greenwich.

Kabla ya Uhuru wa Tanzania bara (Tanganyika),wilaya ya Geita ilikuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 16,638 ambapo nchi kavu ilikuwa ni kilomita za mraba 10,123.94 na maji ilikuwa ni kilomita za mraba 6,514.06. Katika kipindi hicho Geita ilikuwa na idadi ya watu wapatao 371,407. Mnamo mwaka 1975 wilaya ya Geita iligawanywa na kupata wilaya ya Sengerema.Baada ya kugawanywa kwa wilaya hizi mbili, Wilaya ya Geita ilibaki na kilometa za mraba 7,825 ambapo nchi kavu ni kilometa za mraba 6,775 na maji ni kilometa za mraba 1,050.

Mnamo mwaka 2013 wilaya ya Geita iligawanywa tena na kupata wilaya ya Nyang’hwale.Wilaya ya Geita ina Halmashauri mbili ambazo ni “Halmashauri ya wilaya ya Geita na Halmashauri ya Mji“.Halmashuri ya Geita ina ukubwa wa kilomita za mraba 5,366.7(4,316 nchi kavu na 1,050 maji).

Asili ya jina Geita: Neno Geita limetokana na maneno matatu ya kabila la Wayango (Warongo) ambayo ni Akabanga keita abhantu likiwa na maana kupotea kwa mazingara ambayo yalikuwa kwenye mlima huo wa Akabanga keita abhantu uliokuwa ukitumiwa na warongo kama eneo la mitambiko ya jadi.Jina hili la Geita lilikuwa maarufu kutokana na wazungu kushindwa kutamka maneno Akabanga keita abhantu na hivyo kukatisha kuwa Geita hadi leo.Makabila yaliyokuwepo ya Wazinza, Wasukuma,Wasumbwa na Wasubi wakaigiza matamushi ya wazungu Geita na hivyo neno la Akabanga keita abhantu likaanza kupotea polepole hadi leo.

Wilaya ya Geita hupata mvua yenye wastani wa 900mm-1000mm katika tarafa za Busanda na Kasamwa,pia hupata mvua za wastani wa 1000mm-1300mm katika tarafa za Butundwe na Bugando.

shughuli za uchumi kaika wilaya ya Geita ni;kilimo,ufugaji,uvuvi na uchimbaji wa madini ya dhahabu.

UTAWALA KABLA YA WAKOLONI

Kabla ya kuingia kwa wakoloni (Wajerumani na Waingereza) Geita ilikuwa na tawala za asili saba (7) ambazo ni:

UTAWALACHIFU/MTEMI  MAKAO MAKUU
BusambiloLudomya Ng’hweleNyarubele
MsalalaMusa Chasama MbitiKitongo
BuyombeMgunga KadamaBusanda
BuchosaPaulo LukakazaNyakalilo
KharumoAlexander GerevasKharumo
BukoliMganila NongaBukoli
MwingiroNyorobi MapumbaIdetemya Mwingiro

Wakoloni wa kwanza kuingia Geita walikuwa ni wajerumani ambao utawala wao ulikuwa ni wa moja kwa moja(Direct rule) na hivyo kushindwa kabisa kwani wawakilishi wao waliokuwa wakiletwa toka makao makuu Bagamoyo(Pwani) walikuwa wakiuwawa na wenyeji.

Utawala wa pili ulikuwa wa waingereza baada ya vita kuu ya pili ya dunia,ambao wao walitumia utawala usikuwa wa moja kwa moja(Indirect rule) yaani kwa kuwatumia machifu/watemi wa maeneo husika ili kutekeleza azma/malengo yao.

Eneo la mji wa Geita aliwekwa Liwali Petro Nyango ambaye alifanya kazi chini ya utawala wa kwa eneo la mjini.

 BARAZA LA JADI (NATIVE AUTHORITY)

Baraza hili lilikuwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Wilaya(DC) wa kikoloni,liliundwa na watemi na liwali 1.Mwenyekiti wa baraza hilo alitokana na watemi hao.Aidha katibu wa baraza hilo alitokana na watemi au karani kutoka ofisi ya DC.

Makao makuu ya baraza hilo yalikuwa mjini Geita eneo jirani na Benki ya CRDB, kila mtemi alijengewa nyumba ya kupumnzikia na kulala.

MAJUKUMU YA BARAZA HILO

 • Kusimamia ulinzi na usalama
 • Kusimamia shughuli za maendeleo hasusani katika elimu ya msingi,kilimo mkazo ikiwa zao la pamba na mazao ya chakula(Mahindi,Mtama na Uwele) pamoja na barabara.

Historia ya Wahe. Wenyeviti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita

NaJina kamiliMwaka alioanzaMwaka alioonddoka
1.Samwel S. Mabeyo19841988
2.Edward K. Sumuni19881997
3.Said S. Mahuma19972000
4.Jeremia M. Ikangala20002010
5.Musukuma J. Kasheku20102011
6.Elisha H. Lupuga2011

KUPATA NAMBA YA NIDA BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA


KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA


KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA [email protected]

Tags: , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *