NAFASI 9 za Kazi Wilaya ya Ukerewe July 15-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 9 za Kazi Wilaya ya Ukerewe July 15-2024
NAFASI 9 za Kazi Wilaya ya Ukerewe July 15-2024, Kufuatia kutolewa kwa Kibali cha Ajira Mpya chenye Kumb Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe anawatangazia nafasi ya kazi Watanzania wenye sifa na uwezo ya kujaza nafasi tisa (9):-
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA UKEREWE 15-07-2024
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI TANO (5)
MAJUKUMU
- Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji;
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
- Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongezanuzalishaji mali;
- Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalama katika kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.
- Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wako
SIFA ZA WAOMBAJI
Waombaji wanatakiwa wawe wenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form Six) aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.
✅WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI (2)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye regista (incoming correspondence register)
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register);
- Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers)
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
- Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/maja;lada yanayohitajika na watendaji,
- Kurudisha majalada kwenye shubbaka/kabati la majalada (racks/filing cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (File tracking)
SIFA ZA WAOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI). Awe na Stashahada (NTA
level 6) katika fani ya Masjala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa
Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
✅DEREVA WA VIVUKO/MASHUA NAFASI (2)
MAJUKUMU.
- Kufunga na kufungua kamba za mashua/kivuko;
- Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya mashua/vivuko;
- Kupanga abiria au magari kwenye mashua/vivuko;
- Kuendesha na kuongoza mashua/vivuko;
- Kutunza daftari za safari ya mashua/vivuko
- Kuhakikisha kwamba injini za vivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi; na
- Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.
SIFA ZA WAOMBAJI
Kuajiriwa Waliohitimu Mtihani wa Kidato cha Nne, wenye ujunzi wa kuendesha na kutunza mashua/vivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es salaam Marine Institute au Chuo kingine
chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari
kwenye mashua/vivuko.
NGAZI MSHAHARA: Mshahara ni kwa mujibu wa viwango vya mshahara serikalini yaani TGOS A
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za
kazi husika.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards); - “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 26 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe,
S. L.P. 41,
NANSIO/UKEREWE
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
DONWLOAD PDF DOCUMENT
POST: DEREVA VIVUKO DARAJA LA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe More Details |
2024-07-26 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe More Details |
2024-07-26 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe More Details |
2024-07-26 Login to Apply |