RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI 90 za Afisa Uvuvi MDAs na LGAs August 2024

Filed in Ajira by on 03/08/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI 90 za Afisa Uvuvi MDAs na LGAs August 2024

NAFASI 90 za Afisa Uvuvi MDAs na LGAs August 2024,MDAs & LGAs Jobs, MDAs & LGAs August 2024, 90 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024.

NAFASI 90 za Afisa Uvuvi MDAs na LGAs August 2024

NAFASI 90 za Afisa Uvuvi MDAs na LGAs August 2024,MDAs & LGAs Jobs, MDAs & LGAs August 2024, 90 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024.

✅AFISA UVUVI DARAJA LA II (NAFASI
90)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kusimamia uhifadhi wa rasilimali za uvuvi na mazingira yake;
  • Kubuni mbinu na mikakati mbalimbali ya kudhibiti na kuzuia uvuvi haramu kwa mujibu
    wa Sheria ya Uvuvi na Kanuni zake;
  • Kuratibu na kusimamia kazi katika Kituo cha Doria za Uvuvi;
  • Kusimamia doria za baharini, nchi kavu na anga katika maji ya bahari ya ndani na eneo lote la Ukanda wa Uchumi wa Bahari Kuu ‘Economic Exclusive zone’ (EEZ) pamoja na maeneo ya mipakani na viwanja vya ndege;
  • Kuendeleza uvunaji endelevu wa samaki na viumbe wengine wa baharini, maziwa, mito mabwawa na malambo;
  • Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu uvuvi bora;
  • Kufanya kazi zinazohusu masuala ya ushirikishwaji jamii katika shughuli za maendeleo ya uvuvi;
  • Kutoa leseni za uvuvi;
  • Kufanya kazi ya uangalizi wa melini (Fisheries Observers) katika meli za uvuvi;
  • Kuendesha mafunzo ya taaluma ya uvuvi;
  • Kusimamia ukusanyaji wa takwimu za uvuvi pamoja na maduhuli;
  • Kuratibu shughuli za utafiti wa uvuvi;
  • Kutoa ushauri na mafunzo kwa jamii kuhusu uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi; na
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa Kitengo zinazohusiana na fani yake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) katika fani za Sayansi ya Uvuvi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au sifa inayolingana na hiyo kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D

MASHARTI YA JUMLA.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato
    cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali na vyeti vya kitaaluma kulingana na sifa husika kama
    ifuatavyo;.
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate
    Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
    Cheti cha kuzaliwa
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 16 Agosti, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana
kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags: , , ,

Comments are closed.