NAFASI 91 za Afisa Misitu MDAs na LGAs August 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI 91 za Afisa Misitu MDAs na LGAs August 2024
NAFASI 91 za Afisa Misitu MDAs na LGAs August 2024,MDAs & LGAs Jobs, MDAs & LGAs August 2024, 26 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024.
✅AFISA MISITU DARAJA LA II ( FOREST OFFICERS) – NAFASI 91
MAJUKUMU YA KAZI
- Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu;
- Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000;
- Kufanya utafiti wa misitu;
- Kutekeleza Sera na Sheria za misitu;
- Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu;
- Kukusanya takwimu za misitu;
- Kufanya ukaguzi wa misitu;
- Kupanga na kupima madaraja ya mbao;
- Kudhibiti leseni na uvunaji wa misitu/Miti;
- Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya
miti na misitu kwa wananchi; - Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu; na
- Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA:Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato
cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali na vyeti vya kitaaluma kulingana na sifa husika kama
ifuatavyo;.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
Cheti cha kuzaliwa - “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 16 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana
kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: 26 Job Vacancies at MDAs & LGAs Tanzania August 2024., MDAs & LGAs August 2024, MDAs & LGAs Jobs, NAFASI 91 za Afisa Misitu MDAs na LGAs August 2024