NAFASI za Kazi Bunda District Council August 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa kushirikiana na Shirika la Amref Health Africa Tanzania kupitia mradi wa Afya Thabiti anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi kama ilivyoainishwa katika kwenye PDF hapa chini;
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO LA AJIRA BUNDA DC
MASHARTI KWA UJUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha Uraia (NIDA) au namba ya NIDA kwa ambao hawajapata Kitambulisho.
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma yaani nakala ya vyeti vya Kidato cha Nne au Sita pamoja na vyeti vya taaluma (Professional Certificate from respective Board, computer certificate) na picha mbili za rangi za hivi karibuni.
- Testimonial, provisional results, statement of results, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne (Form IV) na Kidato cha Sita (Form VI) havitakubaliwa kabisa.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA na NACTE) na taarifa ya ulinganifu iambatishwe kwenye maombi.
- Waombaji wa nafasi za ajira waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.
- Barua ya maombi iandikwe kwa mkono na kwa lugha ya kiswahili au Kiingereza tofauti na hapo maombi hayo hayatapokelewa.
- Kichwa cha barua ya maombi kitaje nafasi ya kada unayoomba kwa ufasaha.
- Barua ya maombi isainiwe na mwombaji mwenyewe tofauti na hivyo maombi hayo
yatakataliwa. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Waombaji watakaokidhi sifa na vigezo watajulishwa tarehe ya usalli kupitia mbao za matangazo za Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, website ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambayo ni www.bundadc.go.tz, namba zao za simu na anuani walizotumia kwenye barua ya maombi ya kazi.
- Barua zitumwe kwa njia ya Posta au ziwasilishwe kwa mkono masijala ya wazl ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuanzia saa moja na nusu (1:30) asubuhi hadi saa
tisa na nusu (09:30) alasiri.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 05/09/2024.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwa anuani ifuatovyo:-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda,
S.L.P 126,
BUNDA-MARA.