NAFASI za Kazi Chamwino District Council August 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Kazi Chamwino District Council August 2024
Kufuatia idhini ya utekelezaji wa ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2023/2024, kwa kibali chenye Kumb. Na. Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25-06-2024, kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino anawatangazia Watanzania wote wenye sifa za kujaza nafasi za kazi tajwa hapo chini kujisajili na kutuma maombi yao kwa njia ya mfumo wa Ajira Portal.
Nafasi za kazi zinazotangazwa ni hizi zifuatazo:-
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 6
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista (incoming
correspondence register) - Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register)
- Kusambaza majalada kwa Watendaji (action officers)
- Kupokea majalada kwa Watendaji (action officers)
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji
- Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI), aliyehitimu
Stashahada (NTA level 6) katika fani ya utunzaji kumbukumbu kutoka Vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali – TGS C
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 1
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
- Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa;
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika
Idara/Kitengo/Sehemu husika; - Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
- Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha IV au Kidato cha VI wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa
dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGS C kwa Mwezi
✅DEREVA VIVUKO DARAJA LA II – NAFASI 2
KAZI NA MAJUKUMU
- Kufunga na kufungua kamba za mashua/kivuko;
- Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya mashua/vivuko;
- Kupanga abiria au magari kwenye mashua/vivuko;
- Kuendesha na kuongoza mashua/vivuko;
- Kutunza daftari za safari ya mashua/vivuko
- Kuhakikisha kwamba injini za vivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi;
- Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Waliohitimu Mtihani wa Kidato cha Nne, wenye ujuzi wa kuendesha na kutunza mashua/vivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka
miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGOS A kwa Mwezi
✅DEREVA DARAJA II – NAFASI 6
KAZI NA MAJUKUMU
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kufanya usafi wa gari; na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGS B kwa Mwezi
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma; - Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili; - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Shahada au Astashahada, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, -Computer Certificate, – Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 03 Septemba, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili, Kwenda anuani ya; Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino,
S.L.P 1126,
Dodoma
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 1 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, More Details |
2024-09-03 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 6 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, More Details |
2024-09-03 Login to Apply |