NAFASI za Kazi Halmashauri ya Mji Tunduma July 07-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Kazi Halmashauri ya Mji Tunduma July 07-2024
NAFASI za Kazi Halmashauri ya Mji Tunduma July 07-2024,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Mji Tunduma kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenyeKumb Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA 07-07-2024
✅MTENDAJI WA MTAA DARAJA III- (NAFASI 4)
MAJUKUMU YA KAZI
- Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mtaa;
- Katibu wa Kamati ya Mtaa;
- Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa;
- Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa;
- Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika
katika Mtaa; - Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama;
- Msimamizi wa Utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoajiwa njaa na
Umasikini katika Mtaa; - Kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa
kodi; na - Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI)
Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo;Sheria, Elimu ya Jamii,
Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGS B.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi waUmma; - Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/
Wakili; - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa zakuingilia katika
kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi za kazi kwa Waajiri
wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato
cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha
nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua zakisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20/07/2024.
Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Tunduma,
S.L.P. 73,
TUNDUMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemuiliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DONWLOAD PDF YA AJIRA HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA JULY 07-2024
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: NAFASI za Kazi Halmashauri ya Mji Tunduma July 07-2024