RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Halmashauri ya Mji wa Babati July 16-2024

Filed in Ajira by on 16/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Mji wa Babati July 16-2024

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Mji wa Babati July 16-2024

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Mji wa Babati July 16-2024

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Mji wa Babati July 16-2024,TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MJI WA BABATI 16-07-2024.

Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Babati anakaribisha maombi kwa watanzania
wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI (02)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye Regista (Incomming Correspondence Register)
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register)
  • Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers)
  • Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji
  • Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)
  • Kutekeleza kazi zote atakazopangiwa na msimamizi wa kazi

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya masjala kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa compyuta.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C

✅DEREVA DARAJA LA II NAFASI (02)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
  • Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote,
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
  • Kufanya usafi wa Gari,
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria
mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi ya Mshahara ni TGS B

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa
    kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko
    kazini serikalini;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe
    ipasavyo.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza
    (Detailed C.V) yenye anuwani na namba za simu za kuaminika
    pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
    v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia
    kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
    kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za
    matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI
    RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
    vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na
    NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi
    kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia
    walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa
    kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na. CCA. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 29 Julai, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwapamoja na vyeti vya elimu, Anuani ya barua hiyo ielekezwe
kwa;
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji wa Babati,
1 Mtaa wa Halmashauri,
S.L.P. 383,
27103 Bagara, Manyara.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira
(Recruitment Portal)kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz// (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

DONWLOAD PDF DOCUMENT

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.