RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa February 20-2024

Filed in Ajira, Michezo by on 20/02/2024

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 20-02-2024

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 20-02-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 20-02-2024, Nafasi za Kazi Ajira Ludwa DC February 20-2024.

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 20-02-2024

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 20-02-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 20-02-2024, Nafasi za Kazi Ajira Ludwa DC February 20-2024, Tangazo la Kazi Wilaya ya Ludewa 20 February 2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na. FA.228/613/01/025 cha tarehe 08 Disemba 2023 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III- (NAFASI 2)

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI)
  • Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo; Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa
    kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote
    kinachotambuliwa na Serikali.

MAJUKUMU YA KAZI

  • Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kijiji;
  • Katibu wa Kamati ya kijiji;
  • Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Kijiji;
  • Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Kijiji;
  • Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Kijiji
  • Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama;
  • Msimamizi wa Mtekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umasikini katika Kijiji;
  • Kusimamia Ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 20-02-2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 20-02-2024, Nafasi za Kazi Ajira Ludwa DC February 20-2024, Tangazo la Kazi Wilaya ya Ludewa 20 February 2024.

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa 20-02-2024

NGAZI YA MSHAHARA

Ngazi ya mshahara ni TGS B.

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya
    taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili;
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne,
    Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced
    Diploma/Diploma/Certificates, -Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates frombrespective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi waUmma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 05 Machi, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA,
S.L.P 19,
LUDEWA.

Limetolewa na;
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA

CLICK HERE TO APPLY

NAFASI ZA KAZI Mpya Wiki hii, Ludewa District Council, Ludewa Mjini, Ludewa District profile, AJIRA LEO, Njombe to Ludewa km, Nafasi za kazi Ludewa, Historia ya wilaya ya ludewa, Ajira portal, Ajira portal login,
Vijiji vya wilaya ya ludewa,Sekretarieti ya ajira.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Tags: , ,

Comments are closed.