NAFASI za Kazi Kutoka Jeshi la Polisi Tanzania May 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Kazi Kutoka Jeshi la Polisi Tanzania May 2024
NAFASI za Kazi Kutoka Jeshi la Polisi Tanzania May 2024,Majina ya waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi 2024, Ajira za Jeshi la Polisi Tanzania 2024, AJIRA MPYA KUTOKA JESHI LA POLISI MAY 2024.
- SIKU 5 Zaongezwa Maombi ya Ajira za Jeshi la Polisi May 2024
- MFANO Barua Ya Kuomba Kazi Jeshi La Polisi 2024
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anatangaza nafasi za ajira kwa vijana
wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na
Kidato cha nne.
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
- Awe amehitimu kidato cha nne au sita kuanzia mwaka 2018 hadi 2023.
- Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
- Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne (Division I – IV). Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Point) 26 hadi 28.
- Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu (Division I – III)
- Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.
- Awe na urefu usiopunguwa futi tano na inchi nane (5’8”) kwa wanaume, na futi tano inchi nne (5’4”) kwa wanawake.
- Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).
- Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kingereza.
- Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
- Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
- Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya.
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
- Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
- Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
- Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili.
- Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
- Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
- Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8),
Stashahada (NTA level 6) na Astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa wawe na fani zilizoainishwa kwenye tangazo hili. - JINSI ya Kutuma Maombi Ajira za Jeshi la Polisi Tanzania
NAFASI za Kazi Kutoka Jeshi la Polisi Tanzania May 2024
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
- Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (Handwriting) bila kusahau namba za simu na watumie anuani ya
Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA. - Waombaji wote wafanye maombi yao kupitia kwenye mfumo wa Ajira wa Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL)
unaopatikana kwenye tovuti ya Jeshi la Polisi ajira.tpf.go.tz
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 26/05/2024
DONWLOAD PDF DOCUMENT HAPA
Jinsi ya kujiunga na jeshi la polisi tanzania 2024, Vyeo vya jeshi la polisi tanzania, Anuani ya jeshi LA polisi tanzania, Mfumo wa ajira jeshi la polisi tanzania, www.polisi.go.tz ajira 2024, Www polisi go tz ajira login,Jeshi La polisi tanzania ajira 2024, Historia ya jeshi LA polisi tanzania,www.polisi.go.tz ajira,Majina ya waliochaguliwa kujiunga na jeshi la polisi Tanzania,Jinsi ya kujiunga na jeshi la polisi Tanzania, Mkuu wa jeshi la Polisi tanzania.
Historia ya Jeshi la Polisi Tanzania
Jeshi la Polisi la Tanzania lilianzishwa rasmi 25 August 1919 kwa tangazo la Serikaliya Kiingereza lililotoka Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kwa wakati huo likaitwa Jeshi la Polisi Tanganyika.
Lakini jeshi lilianzishwa kisheria kwa Sheria ya uanzishajiwa Jeshi la Polisi ya mwaka 1939 (THE POLICE FORCE AND AUXILIARY SERVICES ACT OF 1939) PRINCIPAL LEGISLATION.
Sheria hii ndiyo inatumika hadi sasa japo imekua ikifanyiwa marekebisho ya mara kwa mara.
Makao Makuu ya Jeshi hilo kulinga na natangazo hilo yalikuwa Wilayani Lushoto Mkoani Tanga chini ya uongozi wa Major S.T Davis.
Baadae Mwaka 1921 Kundi la Wakaguzi Polisi kutoka Ulaya lilifika nchini Tanganyika na kuanzisha Shule ya Mafunzo maalumu ya upolisi huko Mkoani Morogoro ilikukidhi mahitaji yao na kuwa na Askari wenye weledi wakutosha. Pamoja na kuwa na Askari weusi waliofuzu mafunzo lakini bado Askari hao walibaki na vyeo vya chini vya Kipolisi kwani vyeo vya juu vyote walipewa Askari Wazungu.
Jeshi la Polisi la kikoloni lilikuwa na Wanaume pekeyao, hakuna mwanamke aliyepewa nafasi ya kujiungana Jeshi, siyotukwa Watanganyika hata Askari waki koloni wote walikuwa wanaume.
Mafunzo yalilenga kumpa Askari mbinu za kumkandamiza Mwafrika, kuwaminisha kuwa kila walichosema wakoloni ndicho sahihi, ukandamizaji na udhalilishaji kwa Mwafrika ulikuwa mkubwa na ndiyo ilichukua sehemu kubwa ya mafunzo kwa Askari wa Kikoloni.
Askari walifundishwa utii kwa viongozi wakikoloni na ukatili dhidi ya waafrika hasa viongozi wa kikoloni pamoja na machifu. Lengo lilikuwa ni kumtawala Mtanganyika kirahisi.
Watanganyika alitumia silaha za jadi kukabiliana na Askari wa kikoloni, silaha hizo zilikuwa marungu, panga, mikuki, na mishale, pamoja na silaha zilizotengenezwa kwa mawe yaliyochongwa vyema.
Wakoloni waliona ni vyema waanzishe vituo vingi vya Polisi na mwaka 1925 Kituo cha kwanza rasmi cha Polisi nchini kilifunguliwa huko Lupa, Tingatinga Mbeya.
Mwaka 1930 Makao Makuu ya Polisi yalihamishwa kutoka Lushoto Mkoani Tanga kwenda Dar es Salaam. Lengo lilikuwa kuwa na ngome imara ambayo ilisimamia utendaji wa vituo vingine vyote vya Polisi, mawasiliano na maelekezo ya nini kifanyike vituoni yalitolewa kila siku kwa vituo vyote vya Polisi. Radio na barua za kipolisi zilitumika kufikisha ujumbe vikosini.
Baadaye Mwaka 1949 kikosi cha kutulizaghasia, Motorized Company sasa Field Force Unit (F.F.U) kilianzishwa nchini na lengo la kikosi hicho ni kurejesha amani penye vurugu.
Vijana wa kitanganyika walianza kupinga ukandamizaji wa Mkoloni dhidi yao, vijana hao waliongozwa na baadhi ya Askari waliotoka katika vita ya kwanza na ya pili ya Dunia. Hivyo basi iliwalazimu wakoloni kuanzisha kikosi maalum cha kutulizaghasia, pia mwaka huo wa 1949 kwa kuzingatia weledi, Vijana mbalimbali wa Kiafrika kutoka shule mbalimbali za Sekondari Tanganyika walichaguliwa kujiungana Jeshi la Polisi na kuwa Wakaguzi wa Polisi chini ya uangalizi wa muda maalum (Probation Inspectors).
Mwaka 1952 Kikosi maalum cha Mawasiliano (Signals Branch) kilianzishwa Polisi bila kutumia nyaya za simu. Lengo la kikosi hicho ni kuhakikisha Jeshi la Polisi linawasiliana muda wote. Mawasiliano yalisaidia kutoa na kusamba za taarifa kwa haraka zaidi na utekelezaji wake kufanyika na mwaka huo pia Askari wa kike (Women Police) walijiunga na Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa Ms. Payee. Ms. Payee ndiye alikuwa kiongozi wa askari wa kike kwa kipindi hicho.
Mara tu baada ya Tanganyika kupata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961, Jeshi la Polisi lilianza kubadili mwelekeo wake kutoka katika kutumikia Wakoloni na kuanza kuwatumikia wananchi kwa mujibu wa sera za Serikali ya Wananchi wa Tanganyika japo bado lilikuwa na mfumo wa kikoloni. Ilichukua muda kulibadilisha na kulifanya Jeshi la Polisi liwe la kumlinda Mtanganyika na mali zake.
1964 – Hadi sasa : Mabadiliko ya Jeshi kutoka Tanganyika Police kuwa Tanzania Police Force (TPF)
PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA
MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com
Tags: AJIRA MPYA KUTOKA JESHI LA POLISI MAY 2024, Ajira za Jeshi la Polisi Tanzania 2024, Jinsi ya kujiunga na jeshi la polisi Tanzania Anuani ya jeshi la polisi., Majina ya waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi 2024, NAFASI za Kazi Kutoka Jeshi la Polisi Tanzania May 2024
Naipenda kazi ya polisi
Mtandao unasumbua waliongeza siku Tano zinaisha kesho vijana wamejazana stationery kutuma mtandao haufunguki wahusika mnaliona hili
Naipenda kazi ya polisi Sana tena sana
Link haikubali kufnguka tafadhali msaada wenu viongozi
KUOMBA NAFASI YA AJIRA KATIKA KAZI YA JESHI LA POLISI TANZANIA
Naipenda sana kazi uasikali polic
Naipenda sana kazi ya polisi
Napenda Kazi ya kuwa askar polsi
Napenda kujiunga na police
Naipenda sana kaz ta police na nachukia sana uhalifu napenda kuona nchi yangu ina aman mda wote
Yaan system hii unasumbua sana kila nikijaribu kuapply inanisumbua, lakini nahitaji nafasi katika Jeshi la polis la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania
Naipenda sana kazi ya police, naipenda nchi yangu
Naipenda kazi ya polisi nipo tayari kuitumikia mahali popote
Mfumo wa maombi ulkua mzito saana sijui ni network au website ilikua busy saana kulingana na Watu kuingia kwa wingi, Ila kwa niaba ya wote walio fanya jitihada ya kutuma maombi lakini mpaka deadline inafka bila kufanikiwa it’s too much sadness, Ila tusikate tamaa maana amna namna nyingne tena ya kusaidika kuhusu maombi yetu but Inshallah Mwenyezi Mungu atafanya njia kwa wakati mwingne 🙏🏻
Wametangaza ajira lakini hakuna mafanikio yoyote
Nahaidikuwa nikipata nafasi ya kulitumikia taifa langu la Tanzania 🇹🇿🇹🇿🇹🇿 nitakuwa mfano zaidi ya waliopita katika Jeshi la polisi 🇹🇿🇹🇿🇹🇿 sisi tulioko mitaani ndo tunajua wapi Kuna shida tupeni nafasi hizo tunaomba muda uongezwe tena 💪💪💪💪💪💪
Naipenda kazi ya polisi
Maximillian peter kilatsa
S.l.p 443
Buhigwe
24.05.2024
Ndg:
Yah;ombi la nafasi za jeshi la polisi
Naitwa maximillian peter mtanzania wa kuzaliwa,elimu yangu ni muhudumu wa afya ngazi ya jamii nje ya ajila nimependa kuomba nafasi hii kwa ajili ya kulinda raia na mali zao.asante
M.p.kilatsa
Maximillian peter kilatsa
0744676874
mwombaji
Mimi nikijana nilie hitimu kidato cha sita nakupenda kazi ya upolisi toka nilipo zaliwa naomba niwe miongon mwa watakao chaguliwa
I love much police job all is because i dislike some of corruption which still they take place behind the scene and i swear in the name of Allah and my belovely country tanzania when i become a police womani will fight against All that without no fear or wat people a talking about i will forever stand for my country and die for it as a hero girl🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿❤️❤️
jaman hivi mfumo umetulia au ni huku tu nliko?
tujuzane wakuu kama mfumo umetulia wa kuomba ajira jeshi la polisi may2024
Napenda kupata taarifa juu ya maombi tuliyokwisha tuma kwa tayari dirisha limefungwa
Jinsi ya kuagalia mfumo wangu
Napenda kuwa askari police
Napenda kulinda amani ya taifa langu pendwa la TANZANIA
Naipenda kazi ya jeshi la police
Naipend san kaz hiii maan napenda kuitumikia nchi yang na kuilind wapend aman mpoooo
Naipenda kazi ya jeshi la police naomb kupata kazi katika jeshi la police 0713935701
Mimi ally mohamedi ally nimetuma maombi ya upolisi kwani ndio ndoto na matarajio ya maisha yangu naombeni mnisaidie
Maombi ya nafasi yajeshi la kujenga taifa naahidi kuwa mtiifu kwenye kazi hiyo
Wako katika ujenzi was taifa
Naamini katika kazi ya polisi Nina weza kupambana nakila uhalifu .
.
Mimi napenda sana kulinda nchi yangu Tanzania pendwa Kwa kuepuka rushwa na kusimamia haki za binadamu kikamilifu bila kuiangusha nchi yetu yenye upendo na amani hivyo bas kuepuka tu rushwa Hilo Mimi naweza simamia kwasababu nasomea international Relations and Diplomacy . KAZI ya upolisi naipenda sana.
Amani na umoja katika kulijenga taifa la tanzania nipo tayari kuirida amani ya taifa langu katika hali yoyote ile naomba nafasi asanteni
0713540119
Amani na umoja katika kulijenga taifa la tanzania nipo tayari kuirinda amani ya taifa langu katika hali yoyote ile naomba nafasi ya kujiunga na jeshi la polisi tanzania elimu yangu ni kidato cha sita asanteni
0713540119
Naipenda sana kazi ya police naomba nafsi ya kujiunga na jeshi la police ili niweze kutumika nchi yangu na kutetea haki za wanyonge Amina elimu yangu ni kidato cha nne
naipenda sana kazi ya police jaman
Naipenda sana kazi ya police but naomba nafasi zitolewe tena