SELECTION ZA FORM FIVE NA VYUO VYA KATI 2024 BONYEZA HAPA


MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2023/24 BONYEZA HAPA


RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2023/2024 BONYEZA HAPA


JINSI YA KUANGALIA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA FORM FIVE 2024 BONYEZA HAPA


PATA AJIRA MBALIMBALI KILA SIKU BONYEZA HAPA


NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024

Filed in Ajira, Michezo by on 16/03/2024 0 Comments

NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024

NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024, Nafasi za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Chato March 2024, Nafasi za Ajira kutoka Wilaya ya Chato March 2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Chato 14-03-2024.

NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024

NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024, Nafasi za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Chato March 2024, Nafasi za Ajira kutoka Wilaya ya Chato March 2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Chato 14-03-2024.

Kufuatia Halmashauri ya wilaya ya Chato kupata kibali cha ajira mbadala
Kumb.Na.FA.228/613/01/078 cha tarehe 14 Desemba 2023 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu ajira mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato anatangaza nafasi za kazi na
anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kama
zilivyoorodheshwa katika tangazo hili:-

1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI MOJA (1)

SIFA ZA MWOMBAJI

 • Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha nne/sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) Katika moja wapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Msaidizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya
  sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

KAZI ZA MTENDAJI WA KIJIJI

 • Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
 • Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao,kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji.
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Mendeleo ya kijiji.
 • Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya kijiji
 • Kutafsiri na kusimamia sera,sheria na taratibu
 • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi
  katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
 • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika kijiji
 • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
 • Mwenyekiti wa kikao cha wataalaamu waliopo katika kijiji
 • Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
 • Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji na Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

MSHAHARA

 • Kwa kuzingatia viwango vya mshahara ya Serikali ngazi ya Mshahara itakuwa
  TGS B1

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO 14-03-2024 DOWNLOAD PDF

MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE

 • Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
 • Waombaji wenye ulemavu wnahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
 • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe (Email address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
 • Matokeo ya muda (Provisional/Testimonials/Statement of results) havitakubaliwa.
 • Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
 • Wombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
 • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
  katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe iapasavyo.
 • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na Wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyokatika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
 • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
  Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mafunzo mbali
  mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
 • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (NACTE na NACTE)
 • Wasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahausika watachukuliwa hatua za
  kisheria
 • Barua ya maombi itatakiwa iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
 • Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Jumanne, tarehe 21 Machi, 2024.

MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
SLP.116
CHATO -GEITA

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https:portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.

CLICK HERE TO APPLY

NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024, Nafasi za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Chato March 2024, Nafasi za Ajira kutoka Wilaya ya Chato March 2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Chato 14-03-2024.HISTORIA FUPI YA WILAYA YA CHATO

Chato ni mojawapo ya Wilaya tano za Mkoa wa Geita na ilianzishwa rasmi Julai 2006 kutokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Biharamulo.

Wilaya ya Chato ina Halmashauri moja yaani Halmashauri ya Wilaya ya Chato iliyoanzishwa rasmi Julai, 2007.

MIPAKA NA ENEO LA WILAYA

Wilaya ya Chato ipo Kaskazini Magharibi mwa Tanzania kati ya Latitudo 20 15’ hadi 30 15’ Kusini mwa Ikweta na Longitudo 310 hadi 32o Mashariki ya Greenwich.

Wilaya inapakana na Wilaya ya
Muleba Kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Bukombe kwa upande wa Kusini, Wilaya ya Biharamulo kwa upande wa Magharibi na Wilaya ya Geita kwa upande wa Mashariki.

Wilaya ina eneo la kilometa za mraba 3,572 na iko kwenye mwinuko wa kati ya meta 1,135 hadi 1,410 kutoka usawa wa bahari.

IDADI YA WATU

Kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ilikuwa na idadi ya watu 365,127 ambapo kati ya hao 181,368 ni Wanaume na 183,759 ni Wanawake. Idadi ya kaya ni 60,855 sawa
na wastani wa watu 6 kwa kaya.

Wilaya ina watu wenye uwezo wa kufanya kazi wapato 175,261
sawa na asilimia 48 ya wakazi wote.

Hadi kufikia 31 Desemba, 2017 Wilaya inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 420,191 wanaume ni 208,720 na wanawake ni 211,471 (Chanzo cha
taarifa NBS )

UTAWALA

Kiutawala Wilaya ya Chato imegawanyika katika Tarafa 5 za Buzirayombo, Bwanga, Buseresere,
Kachwamba na Nyamirembe.

Kuna Kata 23 zenye Vijiji 115 na Vitongoji 599.

Makao Makuu ya Wilaya ni Chato.

Wilaya ina jimbo moja la uchaguzi, Madiwani 32 ambapo kati yao 23 ni wa
kuchaguliwa kwenye Kata na 8 ni wanawake kupitia viti maalum na Mhe. Mbunge 1.

Dira na Dhima

Mission and Vission,

Dira ya Halmashauri

Kuwa na uchumi imara na endelevu na jamii bora yenye mwanga wa kujiletea maendeleo ifikapo mwaka 2025

Dhamira ya Halmashauri 

Kushirikisha na kushiriki kwa jamii na wadau wote wa maendeleo katika utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa kutumia rasilimali zilizopo

Nafasi za kazi halmashauri 2024, NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO, Nafasi za Kazi halmashauri ya wilaya ya Chato Geita,,Nafasi za kazi halmashauri ya shinyanga, Ajira za watendaji wa vijiji,Nafasi za kazi watendaji wa kata,Nafasi za kazi ngazi ya cheti, Nafasi za kazi watendaji wa vijiji 2024, Ajira portal, NAFASI ZA KAZI Mpya Wiki hii, Nafasi za kazi TAMISEMI,
Nafasi za kazi halmashauri March 2024.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

KUPATA NIDA BURE BONYEZA HAPA

KUOMBA LESENI YA BIASHARA BONYEZA HAPA

KUPATA TIN NUMBER BURE BONYEZA HAPA

KUOMBA LOSS REPORT BURE BONYEZA HAPA

Tags: , , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *