NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024
NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024
NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024, Nafasi za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Chato March 2024, Nafasi za Ajira kutoka Wilaya ya Chato March 2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Chato 14-03-2024.
Kufuatia Halmashauri ya wilaya ya Chato kupata kibali cha ajira mbadala
Kumb.Na.FA.228/613/01/078 cha tarehe 14 Desemba 2023 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu ajira mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato anatangaza nafasi za kazi na
anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kama
zilivyoorodheshwa katika tangazo hili:-
1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI MOJA (1)
SIFA ZA MWOMBAJI
- Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha nne/sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) Katika moja wapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Msaidizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya
sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
KAZI ZA MTENDAJI WA KIJIJI
- Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao,kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji.
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Mendeleo ya kijiji.
- Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya kijiji
- Kutafsiri na kusimamia sera,sheria na taratibu
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi
katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali. - Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika kijiji
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalaamu waliopo katika kijiji
- Kupokea kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji na Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
MSHAHARA
- Kwa kuzingatia viwango vya mshahara ya Serikali ngazi ya Mshahara itakuwa
TGS B1
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO 14-03-2024 DOWNLOAD PDF
MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
- Waombaji wenye ulemavu wnahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe (Email address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Matokeo ya muda (Provisional/Testimonials/Statement of results) havitakubaliwa.
- Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Wombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe iapasavyo. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na Wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyokatika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mafunzo mbali
mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (NACTE na NACTE)
- Wasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahausika watachukuliwa hatua za
kisheria - Barua ya maombi itatakiwa iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
- Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Jumanne, tarehe 21 Machi, 2024.
MUHIMU: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
SLP.116
CHATO -GEITA
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira
(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https:portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
CLICK HERE TO APPLY
HISTORIA FUPI YA WILAYA YA CHATO
Chato ni mojawapo ya Wilaya tano za Mkoa wa Geita na ilianzishwa rasmi Julai 2006 kutokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Biharamulo.
Wilaya ya Chato ina Halmashauri moja yaani Halmashauri ya Wilaya ya Chato iliyoanzishwa rasmi Julai, 2007.
MIPAKA NA ENEO LA WILAYA
Wilaya ya Chato ipo Kaskazini Magharibi mwa Tanzania kati ya Latitudo 20 15’ hadi 30 15’ Kusini mwa Ikweta na Longitudo 310 hadi 32o Mashariki ya Greenwich.
Wilaya inapakana na Wilaya ya
Muleba Kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Bukombe kwa upande wa Kusini, Wilaya ya Biharamulo kwa upande wa Magharibi na Wilaya ya Geita kwa upande wa Mashariki.
Wilaya ina eneo la kilometa za mraba 3,572 na iko kwenye mwinuko wa kati ya meta 1,135 hadi 1,410 kutoka usawa wa bahari.
IDADI YA WATU
Kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ilikuwa na idadi ya watu 365,127 ambapo kati ya hao 181,368 ni Wanaume na 183,759 ni Wanawake. Idadi ya kaya ni 60,855 sawa
na wastani wa watu 6 kwa kaya.
Wilaya ina watu wenye uwezo wa kufanya kazi wapato 175,261
sawa na asilimia 48 ya wakazi wote.
Hadi kufikia 31 Desemba, 2017 Wilaya inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 420,191 wanaume ni 208,720 na wanawake ni 211,471 (Chanzo cha
taarifa NBS )
UTAWALA
Kiutawala Wilaya ya Chato imegawanyika katika Tarafa 5 za Buzirayombo, Bwanga, Buseresere,
Kachwamba na Nyamirembe.
Kuna Kata 23 zenye Vijiji 115 na Vitongoji 599.
Makao Makuu ya Wilaya ni Chato.
Wilaya ina jimbo moja la uchaguzi, Madiwani 32 ambapo kati yao 23 ni wa
kuchaguliwa kwenye Kata na 8 ni wanawake kupitia viti maalum na Mhe. Mbunge 1.
Dira na Dhima
Mission and Vission,
Dira ya Halmashauri
Kuwa na uchumi imara na endelevu na jamii bora yenye mwanga wa kujiletea maendeleo ifikapo mwaka 2025
Dhamira ya Halmashauri
Kushirikisha na kushiriki kwa jamii na wadau wote wa maendeleo katika utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa kutumia rasilimali zilizopo
Nafasi za kazi halmashauri 2024, NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO, Nafasi za Kazi halmashauri ya wilaya ya Chato Geita,,Nafasi za kazi halmashauri ya shinyanga, Ajira za watendaji wa vijiji,Nafasi za kazi watendaji wa kata,Nafasi za kazi ngazi ya cheti, Nafasi za kazi watendaji wa vijiji 2024, Ajira portal, NAFASI ZA KAZI Mpya Wiki hii, Nafasi za kazi TAMISEMI,
Nafasi za kazi halmashauri March 2024.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- EWURA Bei Mpya za Mafuta Tanzania March 06-2024
- USAJILI wa Watahiniwa wa Kujitegemea CSEE NA FTNA 2024
- RITA Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na Vifo
- JINSI ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki RITA
- RITA Utaratibu na Muongozo wa Kuhakiki Vyeti HESLB
- RITA Uhakiki wa Online System 2023/2024
- FAHAMU Kitambulisho Chako Cha NIDA Kilipo
- JINSI ya Kupata Police Loss Report Online
- AINA za Madaraja ya Leseni za Udereva
- JINSI ya Kupata Leseni ya Biashara Online
- JINSI ya Kupata TIN Number Online
- JINSI ya Kulipia Vifurushi vya Azam TV
- OUT yakaribisha maombi ya Udahili Muhula wa Kwanza 2023/2024
- MO Dewji Tajiri namba 12 Barani Africa 2024
- FOMU ya Maombi ya Kujiunga na VETA Tanzania 2024
- ORODHA ya Vyuo vya Ualimu Tanzania
- MFUMO wa Maombi ya Ajira Za Walimu OTEAS 2024/2025
- MSIMAMO NBC Championship 2023/2024
- Haya hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- SHULE 10 Bora Matokeo ya Kidato Cha Nne 2023/2024
- MATOKEO Ya Darasa la Nne 2023/2024
- MATOKEO ya Kidato Cha Pili 2023/2024
- JINSI ya Kuangalia Matokeo Kidato Cha Nne 2023/2024
- ADA za Lipa kwa Airtel Mitandao Yote
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024
- TETESI Za Usajili Yanga SC Dirisha Dogo 2023/2024
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ORODHA ya Vilabu Bora Afrika November 2023 (IFFHS Club Ranking)
- MSIMAMO Kundi D CAF Champions League 2023/2024
- MSIMAMO Wa Kundi B CAF Champions League Standings 2023/2024
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- MSIMAMO NBC Premier League 2023/2024
- WAFUNGAJI Wanaoongoza Magoli NBC Premier League 2023/2024
- KIKOSI cha Yanga SC msimu wa 2023/2024
- RATIBA Kamili Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA ya Mechi za Yanga SC Ligi Kuu ya NBC 2023/2024
- RATIBA Kamili ya Ligi Kuu ya England (EPL 2023/2024)
- KIKOSI cha Simba SC msimu wa 2023/2024
Tags: Nafasi za Ajira kutoka Wilaya ya Chato March 2024, NAFASI za Kazi Kutoka Wilaya ya Chato 14-03-2024, Nafasi za Mtendaji wa Kijiji Wilaya ya Chato March 2024, Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Chato 14-03-2024.