RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Manispaa ya Iringa July 2024

Filed in Ajira by on 21/07/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Kazi Manispaa ya Iringa July 2024

NAFASI za Kazi Manispaa ya Iringa July 2024

NAFASI za Kazi Manispaa ya Iringa July 2024

NAFASI za Kazi Manispaa ya Iringa July 2024,Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Iringa 20-07-2024,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

✅MWANDISHI MWENDESHA OFFISI DARAJA II- (NAFASI 5)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri;
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza ;
  • Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake
    na ratiba za kazi zingine;
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
  • Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali;
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi;
  • Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi; na
  • Na kazi zingine utakazo pangiwa na mwajiri wako.

SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI)
Awe amehitimu mafunzo ya Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili.

Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maeneo 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, Email na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGS C

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa
    Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili;
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika
    kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato
    cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
    kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 01/08/2024.

Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi wa Halmashauri,
Manispaa ya Iringa,
S.L.P. 162,
IRINGA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.