NAFASI za Kazi Manispaa ya Ubungo August 01-2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Kazi Manispaa ya Ubungo August 01-2024
NAFASI za Kazi Manispaa ya Ubungo August 01-2024, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo amepokea Kibali cha Ajira Mbadala kutoka kwa Katibu Mkuu OR – Utumishi chenye Kumb.Na. FA. 228/613/01/D/040 ya tarehe 09.07.2024.
Hivyo anapenda kuwatangazia Watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada moja (1) kama ilivyoainishwa kwa kuzingatia sifa tajwa hapo chini: –
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 1
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuorodhesha barua zinzoingia masjala kwenye rejista (incoming correspondence
register); - Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing correspondence register);
- Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers);
- Kupokea majalada yanayorudi masijala toka kwa watendaji;
- Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji;
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada
( racks / filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa - Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe Muhitimu wa Kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada au NTA level 6 ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali -TGS C.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 – 45
- Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
- Barua ya muombaji ioneshe anuani anayotumia kwasasa pamoja na namba ya simu
ikiambatana na:- - Nakala za vyeti vya taaluma.
- Nakala ya vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne, sita na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa na kazi husika.
- Maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu zinazopatikana na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Picha mbili (2) za “Passport Size” za hivi karibuni.
- Kitambulisho cha Taifa au namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Waombaji waliowahi kupatikana na kosa la jinai hawatafikiriwa
- “Testmonies”, “Provisional Result”, “Statement of Results” hati ya matokeo ya Kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULT SLIPS
HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE). - Waombaji waliostaafishwa/ kuachishwa kazi katika
Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama ana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Waombaji wenye sifa zaidi ya zilizotajwa hapo juu maombi yao hayatafikiriwa.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 09 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,
S.L.P 55068,
DAR ES SALAAM.
Maombi yote yatumwe kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.