RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Mji Nanyamba August 02-2024

Filed in Ajira by on 02/08/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Kazi Mji Nanyamba August 02-2024

NAFASI za Kazi Mji Nanyamba August 02-2024

NAFASI za Kazi Mji Nanyamba August 02-2024

NAFASI za Kazi Mji Nanyamba August 02-2024, Halmashauri ya Mji Nanyamba imepokea kibali cha Ajira mpya chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024, chenye nafasi ya Mtendaji wa Mtaa III (4) na Msaidizi wa Kumbukumbu II (3) kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo :-

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II NAFASI 3

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye regista (incoming
    correspondence register).
  • Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register)
  • Kusambaza majalada kwa Watendaji (Action Office).
  • Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji.
  • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji.
  • Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling cabinets)Bau mahali pengine yanapohifadhiwa.
  • Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking).

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) aliehitimu mafunzo ya
stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C1

✅MTENDAJI WA MTAA III– NAFASI 4

KAZI NA MAJUKUMU YA MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III

  • Katibu wa Kamati ya Mtaa.
  • Mtendaji Mkuu wa Mtaa.
  • Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na
    Halmashauri katikaMtaa.
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu mipango ya maendeleo katika Mtaa.
  • Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria
    nyingine zinazotumika katika Mtaa.
  • Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya ulinzi na usalama.
  • Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa naumaskini katika mtaa.
  • Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza
    kumbukumbu zawalipa kodi wote.
  • Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa.
  • Kuwajibika kwa Mtendaji wa Kata.

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya
Astashahada (Cheti) cha NTA Level 5 katika moja ya fani zifuatazo: Utawala,
Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya jamii na Sayansi ya
Jamii kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS B.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na
    usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
    kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae)
    yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (Email address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingilia katika
    kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri
    wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
    HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Wakatakao kidhi Sifa zinazotakiwa ndio pekee watakaoitwa katika Usahili.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15/08/2024

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Nanyamba,
S.L.P 1490,
NANYAMBA-MTWARA.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.