NAFASI za Kazi Nsimbo District Council August 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Barua yenye Kumb.Na.FA.97/228/01/09 ya tarehe 25.06.2024.
Hivyo, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi 1 ifuatayo:
✅MPISHI DARAJA LA II (NAFASI 01)
KAZI NA MAJUKUMU
- Kufanya usafi wa jiko;
- Kupika vyakula vya aina mbalimbali;
- Kuhakikisha vyombo vya kupikia vinakuwa safi
- Kutayarisha orodha ya vyakula vya mlo kamili (balanced diet);
- Kupika vyakula vya kitaalam;
- Kuhakikisha chakula kinaandaliwa kwa muda muafaka;
- Kuahakikisha usalama wa jiko na chakula; na
- Kutekeleza majukumu mengine utakayopangiwa na msimamizi wako
SIFA ZA MWOMBAJI.
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) . Awe na Astashahada/cheti (Technician Certificate) ya fani ya Mapishi (Food Production/ Culinary Arts) kutoka Chuo chochote kinachotambulika
na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa wale waliokokazini Serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuhainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya
taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma; - Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo; - Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu naTaaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Certificates, – Cheti cha mtihaniwa Kidato cha IV na VI,-Computer Certificate;
- “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi;
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 watarehe 30 Novemba,2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29/08/2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazii liyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwekwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,
SLP 688
NSIMBO – KATAVI
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa (‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazohili HAYATAFIKIRIWA.