NAFASI za Kazi Sengerema District Council August 2024
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA
NAFASI za Kazi Sengerema District Council August 2024
NAFASI za Kazi Sengerema District Council August 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema amepokea kibali cha kutekeleza Ikama na Bajeti kwa Ajira Mpya kwa mwaka wa fedha 2023/2024 chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema anawatangazia wananchi wote ambao ni Raia wa Tanzania wenye sifa kuomba nafasi zilizoorodheshwa hapa chini: –
✅DEREVA DARAJA LA II-(NAFASI 4)
MAJUKUMU YA DEREVA
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari na vi. Kufanya usafi wa gari
SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI), Awe na Leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B 1.
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II (NAFASI 8)
MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri
- Kupokea Wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa za kumbukumbuka za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/ Kitengo/ sehemu husika
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe Amehitimu Elimu ya kidato cha Nne (IV) au kidato cha sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na kingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile; Microsoft Word, Microsoft Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C 1.
✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III (NAFASI 3)
MAJUKUMU
- Afisa Masuuli na Mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
- Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
- Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalama katika kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji:
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji Mkuu wa Kata.
- Pamoja na kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wake.
SIFA ZA KUAJIRIWA
Waombaji wanatakiwa wawe wenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form Six) aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B.
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMU DARAJA II (NAFASI 5)
MAJUKUMU
- Kutafuta kumbukumbu nyaraka /majalada yanayohitajika na Watendaji /Action Officers
- Kudhibiti upokeaji na uandikishaji wa kumbukumbu / nyaraka
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista (incoming corresponding registers)
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga nyaraka mbalimbali katika masjala kulingana na somo husika (clarification and indexing)
- Korodhesaha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing corresponding register)
- Kusambaza majalada kwa Watendaji/ Action Officers
- Kufuatiliaji mzunguko wa majalada ndani ya taasisi
- Kurudisha majalada kwenye kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa
- Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa Watendaji/ Action Officers
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha sita (Form VI) aliehitimu mafunzo ya Stashahada /Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kompyuta.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C 1.
MASHARTI KWA UJUMLA.
- Mwombaji anatakiwa awe Raia wa Tanzania na mwenye umri usiozidi miaka 45.
- Mwombaji aambatishe cheti cha kuzaliwa
- Mwombaji ambaye tayari ni Mtumishi wa Umma na amejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na alizonazo, apitishe barua yake ya maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wake.
- Mwombaji aambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatishwe na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya Kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
✓ Certificates
✓ Diploma
✓Cheti cha mtihani wa Kidato cha nne au kidato cha sita
✓ Computer Certificate
✓ Vyeti vya kitaaluma (Professional certificate from respective boards)
✓ Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni. - Testmonial, “Provisional Results”, “Statement of Results”, hati matokeo
za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA - Mwombaji aliyesoma nje ya Tanzania ahakikishe vyeti vyake vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
- Mwombaji wa nafasi ya Ajira aliyestaafishwa/kuachishwa kazi katika Utumishi wa Umma haruhusiwi kuomba isipokuwa kama anakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Mwombaji wa kazi ambaye tayari ni mwajiriwa katika nafasi ya kuingilia aliyeko katika Utumishi wa Umma asiombe kwa kuzingati maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachuliwa hatua za kisheria.
- Maombi yote yaombwe kwenye Mfumo wa (Recruitment portal) kupitia anuani ifuatayo:- Kielekitroniki wa Ajira http://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment portal)
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu (kwa njia ya Posta/ Mkono) na kwa kutofuata utaratibu uliobainishwa katika tangazo hili Hayatapokelewa.
Kumbuka Kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi katika Mfumo iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu vilivyothibitishwa na Mwanasheria, Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA,
5 BARABARA YA BOMANI,
33381 NYATUKARA,
S.L.P 175
SENGEREMA
Mwisho wa kupokea maombi ya kazi katika mfumo ni tarehe 20 Agosti,
2024.