RATIBA YA LIGI KUU YA NBC 2024/2025 TAZAMA HAPA


INEC RATIBA YA UBORESHAJI WAPIGA KURA 2024/2025 HAPA


INEC KUITWA KWENYE USAILI 2024/2025 TAZAMA HAPA


AJIRA MPYA KILA SIKU TAFADHALI BONYEZA HAPA


JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP HAPA


NAFASI za Kazi Tanganyika District Council August 2024

Filed in Ajira by on 23/08/2024
SHARE THIS POST:

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA

NAFASI za Kazi Tanganyika District Council August 2024

NAFASI za Kazi Tanganyika District Council August 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amepokea Kibali cha Ajra mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 ya tarehe 25.06.2024.

Hivyo, anawatangazia wananchi wote wenye sifa za kujaza nafasi 2 zifuatazo; –

✅MPISHI DARAJA LA II – NAFASI 2

MAJUKUMU YA KAZI:

  • Kufanya usafi wa Jiko;
  • Kupika vyakula vya aina mbalimbali;
  • Kuhakikisha vyombo vya kupikia vinakua safi;
  • Kutayarisha orodha ya vyakula vya mlo kamili;
  • Kupika vyakula vya kitaalam;
  • Kuhakikisha chakula kinaandaliwa kwa muda muafaka;
  • Kuhakikisha usalama wa jiko na chakula; na
  • Kutekeleza majukumu mengine utakayopangiwa na msimamizi wako.

SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata cheti. Awe na Astashahada/cheti (Technician Certificate) ya fani ya mapishi (food production/Culinary Arts) kutoka
chuo chochote kinachotambulika na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA TGS C.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI:

  • Mwombaji awe Raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45;
  • Mwombaji aambatishe nakala ya vyeti vya Elimu ya Sekondari, taaluma na nakala ya cheti cha
    kuzaliwa vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili. Waombaji watakaowasilisha “Result Slip,
    Statement of Results, Provisional Results au Transcripts” havitakubalika.
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye
    anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail address)
    pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya kazi kwa Waajiri wao na waajiri
    wajiridhishe ipasavyo;
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE);
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama
    wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi;
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za
    Nchi;
  • Waombaji watakaokidhi vigezo wataitwa kwenye usaili;

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 29.08.2024;

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya
elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,
S.L.P. 1,
MPANDA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

SHARE THIS POST:

Tags:

Comments are closed.